Feb 16, 2015

Misri yaishambulia ISIS Libya

Rais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri akiwafariji wakuu wa Kanisa la Coptic
Wakuu wa kanisa la Coptic Taarifa kutoka Misri zasema kuwa, ndege za kijeshi zimewashambulia wapiganaji wa jihadi nchini Libya kwa mabomu, baada ya kutolewa kwa mkanda wa video ulioonyesha wakristo wa Misri wa madhehebu ya Coptic wakikatwa shingo.

Jeshi la Misri linasema kuwa limelenga kambi za Islamic State, kituo cha mafunzo na maghala ya silaha, katika shambulizi hilo la mapema leo alfajiri.

Walioshuhudia wanasema kuwa, mji wa Derna ulioko mashariki mwa Libya na ambao umetekwa na wapiganaji wa jihadi ndio ulioshambuliwa vibaya.

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, amesema kuwa mashambulio hayo ya angani ni jibu kwa wapiganaji hao ambao walitoa mikanda hiyo ya video hapo jana jumapili ilioOnyesha waumini kumi kati ya 21 waliotekwa nyara wakichinjwa.
Waumini hao wa madhehebu ya Coptic walikuwa wametekwa nyara majuma kadha yaliyopita.

Jeshi la Misri limetoa taarifa kwa vyombo vya habari inayosema kuwa raia wa taifa hilo walioko mbali ama karibu, wanafaa kuelewa kuwa wana jeshi la taifa linalowalinda kokote waliko. 

Taarifa kutoka Misri zasema kuwa, ndege za kijeshi zimewashambulia wapiganaji wa jihadi Nchini Libya kwa mabomu, baada ya kutolewa kwa mkanda wa video ulioonyesha wakristo wa Misri wa madhehebu ya Coptic wakikatwa shingo.

Jeshi la Misri linasema kuwa limelenga kambi za Islamic State, kituo cha mafunzo na maghala ya silaha, katika shambulizi hilo la mapema leo alfajiri.

Walioshuhudia wanasema kuwa, mji wa Derna ulioko mashariki mwa Libya na ambao umetekwa na wapiganaji wa jihadi ndio ulioshambuliwa vibaya.
Waumini wa kanisa la Coptic wakiandamana nje ya mojawepo ya makani yao Misri

Maandishi yaliyowekwa katika video hiyo yanaonyesha walilengwa kwa sababu ya dini yao. 

Misri imetangaza wiki moja ya maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo vya watu hao.

Mamlaka ya Kiislam inayoongoza nchini Misri,-- Al Azhar -- imeshutumu mauaji hayo na kuyaita ni ya "kinyama". Maelfu ya Wamisri wamekuwa wakivuka mpaka kwenda kutafuta kazi nchini Libya licha ya ushauri wa serikali yao ya Misri kuwakataza wasiende huko.

0 comments:

Post a Comment