Ujumbe wa Ijumaa

Neema Za Allaah Hazihesabiki

Mola wetu Mtukufu Amemuumba mwanaadamu katika umbo bora lisilomithilika na kiumbe chochote. Naye ameumbwa kwa kutumia udongo uliopulizwa roho itokayo kwa Mola Mlezi.
 
Akamjaalia mwanaadamu ni mwenye kupata shida, mitihani, mtenda dhambi na mwenye kupata maradhi. Hakusita hapo Mola wetu Mtukufu, bali Akajaalia mlango wa pili wa kutokea kwenye mashaka ya dunia; Akajaalia kuwepo starehe, utulivu, toba na afya. Basi ni kwa neema zipi mwanaadamu anaweza kumlipa Mola wake!?
 
Tutambue kwamba hii roho tuliyokuwa nayo yatosha kuwa ni sababu ya kushukuru neema za Mola Mlezi kwa vitendo na kauli. Tusisahau wapi tulipotoka na wapi tunaelekea, hatukuwa chochote miaka 100 iliyopita. Basi ni nani kati yetu alikuwa na uhakika kwamba atadhihiri duniani kwa jina na umbo lake kabla ya kuzaliwa? Kuwa na adabu kwa kumcha Mola wako!
 
Muislamu yupo juu ya mgongo wa ardhi akiruzukiwa kila chenye manufaa na yeye, ni mwenye kula akapata njia ya kutolea uchafu, na siku uchafu unaposhindwa kutoka ndani ya tumbo ndio unaelewa umuhimu wa neema ya kuyeyusha chakula kwenye mwili. Ameumba kila kitu kwenye kiwango maalumu, kwani tumbo likiyeyusha kupita kiwango, mwanaadamu ataugua maradhi ya tumbo la kumuendesha. Hivyo, kumbuka na yazingatie maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
{{Na mkihesabu neema za Allaah hamtaweza kupata idadi yake. Hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu.}} [An-Nahl: 18]
 
Basi elewa ndugu yangu, kwamba sisi si chochote si lolote zaidi ya tone la manii lililoengwa engwa hadi likafikia miezi tisa likaweza kutoka kwa sura ya mwanaadamu. Ndani ya tumbo, Mola wetu Mlezi Alitulinda na wala hatukuhitaji askari, jeshi, polisi, ultimate security au mwengineye. Ukatoka kwa ukenya wa kilio cha juu ukiomba msaada kwa mama yako. Ukafikia baleghe ukaweza kuoa/kuolewa na sasa kwa Qadar ya Mola unaweza nawe kupata mtoto. Aliyekuwa mbabe kati yetu azihesabu neema ngapi zimepita baina ya kuzaliwa kwake hadi hivi sasa, kisha aangalie ni kwa kiwango gani ataweza kuzishukuru neema hizo. SubhaanaLlaah! Yuko umbali gani mwanaadamu kwa kuzitilia maanani neema za Mola wake?
 
Ugeuze uso wako, uangalie mbingu ilivyotanda na ardhi ilivyotandikwa, kisha useme kwamba Mola wako amekutupa. Rizki zako Akazimimina kutoka mbinguni na Akazichimbua kutoka ardhini. Ni kipi basi katika chakula chako kitokacho nje ya mfumo huu? Basi kwa Kiburi Chake Mola Mlezi Anastahiki kuyaambia makundi ya wanaadamu na majini:
{{Enyi jamii ya majini na watu! Kama mtaweza kupenya katika mbingu na ardhi (ili mkimbie Nisikupateni), basi penyeni (Nikuoneni)! Hamtapenya ila kwa nguvu (Zangu. Nikikupeni nguvu hizo mtaweza).}} [Ar-Rahmaan: 33]
 
Tumcheni Mola wetu kwa kila kitu, kwa dogo na kubwa, kwa tunayoyajua na tusiyoyajua. Tutende mema kabla ya kutufika yale yasiyoweza kuhimili miili yetu. Wahenga wanatuambia: "Kijua ndi hichi usipouanika utaula mbichi."

*********************************************************************************************************
 ZITUMIE SIFA KUMI
Anasema Allaah سبحانه وتعالى :

((إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ وَالْحَافِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَالْحَافِظَاتِ وَالذَّاكِرِينَ اللَّهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا))

((Hakika Waislamu wanaume [wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu] na Waislamu wanawake [wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu], na Waumini wanaume [wanaoamini vizuri nguzo za Iymaan] na Waumini wanawake [wanaoamini vizuri nguzo za Iymaan], na wanaume wanaotii na wanawake wanaotii, na wanaume wasemao kweli na wanawake wasemao kweli, na wanaume wanaosubiri, na wanawake wanaosubiri, wanaume wanaonyenyekea na wanawake wanaonyenyekea, na wanaume wanaotoa [Zaka na] sadaka  na wanawake wanaotoa [Zaka na] sadaka, na wanaume wanaofunga [Swawm] na wanawake wanaofunga [Swawm] na wanaume wanaojihifadhi tupu zao na wanawake wanojihifadhi tupu zao, na wanaume wanaomtaja Allaah kwa wingi na wanawake wanaomtaja Allaah [kwa wingi], Allaah Amewaandalia msamaha na ujira mkubwa)) [Al-Ahzaab:35]

Kama tunavyoona katika hiyo Aayah tukufu kuwa hizo ni sifa kumi Alizozitaja Allaah سبحانه وتعالى ambazo pindi Muislamu akizimiliki atapata kusamehewa makosa yake kupata ujira mkubwa kutoka kwa Mola Mtukufu. Hivyo kila mmoja wetu apime nafsi yake na kuhesabu kama yumo katika kumiliki sifa hizi zote kumi.  Ikiwa mtu anamiliki sifa mojawapo au zaidi yake, basi ajitahidi kuzifanyia kazi zote ili akamilishe kuwa na sifa hizo.
Tutaweka maelezo katika kila sifa moja ili tuweze kufahamu maana yake huku tukimuomba Allaah سبحانه وتعالى Atuwezeshe kuzichuma sifa zote, na Atutakabalie amali zetu. Aamiyn. 

Sababu ya kuteremshwa Aayah hii:


 عن عبد الرحمن بن شيبة، سمعت أم سلمة زوج النبي صلى الله عليه وسلم تقول: قلت للنبي صلى الله عليه وسلم: ما لنا لا نُذْكَرُ في القرآن كما يذكر الرجال؟ قالت: فلم يَرعني منه ذات يوم إلا ونداؤه على المنبر، قالت، وأنا أسَرّح شعري، فلففت شعري، ثم خرجت إلى حُجْرة من حُجَر بيتي، فجعلت سمعي عند الجريد، فإذا هو يقول عند المنبر: ))يا أيها الناس، إن الله يقول:   إن المسلمين والمسلمات والمؤمنين والمؤمنات )) إلى آخر الآية  (الإمام أحمد)

Imetoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Shaybah kwamba: Nimemsikia Ummu Salamah رضي الله عنها  mke wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akisema:  Nilimwambia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم: kwa nini sisi wanawake hatutajwi (sana) katika Qur-aan kama wanavyotajwa wanaume? Kisha siku moja bila ya mimi kutambua, alikuwa akiita katika Minbar nami nilikuwa nikichana nywele zangu, nikazifunga nywele zangu nyuma kisha nikaingia chumbani katika vyumba vya nyumba yangu, nikaanza kusikiliza, naye alikuwa akisema kutoka katika Minbar: ((Enyi watu! Allaah Anasema: “ Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake na Waumini wanaume  na Waumini wanawake…)) mpaka mwisho wa Aayah. [Imaam Ahmad] 

Sifa ya Kwanza:

((نَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ))

 ((Hakika  Waislamu wanaume [wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu] na Waislamu wanawake [wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu]))

Zinatambulika nguzo za Kiislamu kuwa ni tano. Muislamu anapaswa kuzitimiza zote ili ukamilike Uislamu wake. Nguzo hizo zimetajwa katika Hadiyth ifuatayo:

 عبدالله بن عمر  قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم (( بُنِـيَ  الإِسْلاَمُ علـى خَمْسٍ: شَهادَةِ أنْ لا إِلٰهَ إلا الله وأنَّ مُـحَمَّداً رَسُولُ الله وإِقامِ الصَّلاَةِ وإِيتاءِ الزَّكاةِ وَحَجِّ البَـيْتِ وَصَوْمِ رَمَضَانَ)) البخاري

Kutoka kwa ibnu 'Umar ambaye amesema: Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema: ((Uislamu umejengeka kwa matano; Kushuhudia [na kukiri kwa moyo]  kwamba hakuna ilaah [mungu mwabudiwa wa haki] isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Allaah na kuswali [Swalah tano], kutoa Zakaah, kuhiji katika Nyumba [Makkah] na kufunga ]mwezi wa] Ramadhaan)) [Al-Bukhaariy]

************************************************************************************************************WATU AINA SABA WATAKAOKUWA KATIKA KIVULI CHA ALLAAH SIKU YA KIYAMA

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kuna watu saba (7) ambao Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) atawafunika katika kivuli chake katika siku ambayo kutakuwa hakuna kivuli isipokuwa kivuli chake Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)”:

1.    Kiongozi Muadilifu;
2.    Kijana aliyekulia katika kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala);
3.    Muislamu ambaye moyo wake umesehelea katika msikiti;
4.    Watu wawili wapendanao kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), Kukutana kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na kuachana kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala);
5.    Mwanaume aliyeitwa na mwanamke mrembo kwa kutaka kufanya matendo ya haramu na akasema, “La hakika mimi namuogopa Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala)”.
6.    Mtu anayetoa sadaka kwa mkono wa kulia na wa kushoto usijue kitu kilichotendeka (atoae sadaka kwa siri bila ya wengine kujua kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), na
7.    Mtu anayemkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa faragha na huku macho yake yakatokwa na machozi.”
    (Al-Bukhaariy na Muslim)


Katika Hadiyth hii nzuri Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kazungumzia kuhusu vitu vidogo vya ‘Ibaadah ambavyo ujira wake ni mkubwa mno: kivuli katika siku ambayo kutakuwa hakuna kivuli isipokuwa cha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Hii inaweza kuonekana kuwa si jambo kubwa katika mara ya kwanza utakaposoma, lakini ukidhamiria katika Hadiyth ifuatayo; “Katika siku ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) atawafufua viumbe vyake vyote, jua litashushwa karibu sana na watu ambapo kutaachwa tofauti ya maili moja baina ya jua na watu ardhini. Watu watatopea katika jasho kulingana na amali zao, wengine mpaka kwenye vifundo vya vya miguu, wengine mpaka kwenye magoti yao, wengine mpaka kwenye viuno vyao na wengine watakuwa na hatamu ya jasho na, wakati yalivokuwa yanasemwa haya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliweka mkono mbele ya mdomo wake.” Imesimuliwa na Al-Miqdaad bin Aswad na imekusanywa katika Swahiyh Muslim - Juzuu ya nne (4), ukurasa wa 1487-8, nambari 6852.

Na katika Hadiyth nyengine, watu wengine watatopea katika jasho “Sawa na urefu wa mikono sabini (70) katika dunia” (Al-Bukhaariy na Muslim)

Nani atataka zaidi ya kuwa katika kivuli na hifadhi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) katika siku hii. Wacha tu tuchunguze sasa sifa na fadhila za haya makundi saba (7) ya watu ambao wanastahiki na kuadhimikiwa na nafasi hii katika siku ambayo binaadamu wote watakusanyika.

  1. “Kiongozi Muadilifu…” Sheria/Haki katika Uislamu ni muhimu sana na ni kitu ambacho kila Muislamu Kiongozi na waongozwa lazima wafuate katika kila kitu bila ya hitilafu yoyote. Sheria ni kumpa kila mtu haki anayestahiki. Waislamu au wasio waislamu, ndugu au mgeni, rafiki au adui. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema: “Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na ucha Mungu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu Anazo khabari za mnayoyatenda.” [Al-Maaidah: 8]

Hata kama tunakubali katika kanuni, tunasahau haraka kwenye kufuata. Ndio maana unaona tukizungumza kuhusu  marafiki zetu na watu walio karibu nasi, tunawasifia kupita kiasi, na tukizungumza kuhusu watu kinyume na hao, hatusemi hata jema moja lao na tunayakumbuka au kuyataja mabaya yao tu. Hii imetolewa na kutupwa kabisa katika sheria/haki ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anaipenda na hutoa ujira au thawabu kubwa mno kwaye, kama ilivotajwa katika Hadiyth ifuatayo: “Yule mtenda sheria atakuwa katika kiti cha enzi kwenye mkono wa kulia wa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) – na hakika mikono yote ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) ipo kulia (haki) kwa wale ambao waadilifu wa sheria katika utawala wao, baina ya familia zao na kila kitu ambacho wamepewa mamlaka [Muslim].


Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuagiza Abdullaah bin Mas’uud sehemu iliowazi katika mji wa Madiynah baina ya makazi na bustani ya mitende ya Answaar na aliposema Banu ‘Abd bin Zuhrah, “Watoe hapa kwetu watoto wa Umm ‘Abd (Ibn Mas’uud), akajibu, “Kwanini Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) amenileta mimi. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) hapendi wala hawarehemu watu baina yenu ambao hawatoi haki kwa watu walio dhaifu. [At-Tirmidhiy]

Kutekeleza Sheria kwa haki na uadilifu ni muhimu sana kwa mtawala yoyote, madhali yeye ndio mshika hatamu wa watu wake na yeye ndio mtoa haki wa mwisho katika sehemu husika, Kwa sababu hii, mtawala amepewa nafasi muhimu sana kama mmoja katika watu saba ambao watatunikiwa kivuli cha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) siku ya Qiyaamah.

  1. “Kijana aliyekulia katika kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)… Mwanachuoni mkubwa Ayyuub as-Sakhtiyaaniy (aliyefariki mwaka 131H) amesema, “Kutokana na mafanikio anayokuwa nayo kijana, Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anamuongoza kuwa mwanachuoni wa Sunnah.” Hasan – Imesimuliwa katika Sharh Usuul as-Sunnah ya Imaam al-Laalikaa’iy (Namba 30).


Kweli, ni baraka iliyoje kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa kijana ambaye ameongozwa kwenye ibada na akawa na urafiki au uongozo mzuri kwenye mambo mema, kwani kama tunavojua kuwa ni katika ujana wa mtu ambapo hukabiliwa na vishawishi vya dunia na huwa rahisi kuteleza kwenye njia ya Uislamu. Hii inakuwa dhihirifu pale tunapoana kwenye jamii zetu na tunaona hadaa nyingi za kidunia, kama muziki, michezo, vilabu mbali mbali visivo vya kheri, mambo ya fasheni na kadhalika. Hivi vyote huwa vimelenga au mlengwa mkuu katika mambo hayo tuliyoyataja hapo juu ni vijana. “Ujana huwa mara moja tu!” huwa wanaambiwa, na ndio maana Waislamu wengi siku hizi wanapoteza ujana wao kufikiri kuwa wataswali, watavaa Hijaab na kwenda kuhiji na kadhalika pale watakapofikia umri wa uzee, kama vile wana uhakikisho wa maisha marefu kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)! Ewe ndugu yangu Muislamu ni kiasi gani tunajali wasia wa mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema: “Chukua faida ya mambo matano (5) kabla ya matano (5): ujana wako kabla ya uzee wako, afya yako kabla ya maradhi yako, mali yako kabla ya ufukara wako, faragha yako kabla ya wakati utakaoshughulishwa na mambo mbali mbali, na maisha yako kabla ya kifo chako.” [Al-Haakim]
  1. Muislamu ambae moyo wake umesehelea (umeambatana) katika msikiti… Kuna msisitizo mkubwa katika Sunnah kwa Muislamu mwanaume kuswali msikitini na malipo yake ni ni makubwa mno. Sio tu inamwezesha mtu astahiki kivuli cha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) siku ya Qiyaamah, bali pia “…kila hatua anayochukua kuelekea msikitini hunyanyuliwa daraja moja na hufutiwa dhambi moja. Wakati akiswali, Malaika hawaachi kumuombea madhali yuko katika sehemu ya ibada na husema, Ewe Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma  mrehemu mja wako huyu, Ewe Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mhurumie mja wako huyu…” [Al-Bukhaariy]

Hadiyth zote zinazowahamasisha wanaume kusehelea misikitini hazimaanishi wala hazikusudii kumuongoza mmoja kufikia timamu ya kwamba Uislamu ni Dini ambayo inatakiwa itekelezwe misikitini tu, kama watu wengi wanavofikiria. Misikiti inatakiwa iwe katika moyo wa jamii ya Kiislamu, na jukumu la wale wahusika wa msikiti ni kubwa na zito. Wao ndio wahusika wakuu wa kukaribisha stara kwa Waislamu, kuliko kuwa uwanja wa siasa na kitega uchumi kama ilivokuwa misikiti mingi siku hizi. Na tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atuepushe na mambo kama haya kutokea!
  1. “Watu wawili wapendanao kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), wakakutana kwa ajili ya Mola wao na wakatengana kwa ajili ya Mola wao…” Kuwa na upendo wa dhati kwa jili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) ni moja ya milango mitukufu kuelekea kwenye mazuri ya huko akhera na ni chanzo cha kuonja uzuri wa Imani katika dunia hii. Kupendana kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) inamaanisha Muislamu anatakiwa ampende Muislamu mwenzake kwa ajili ya usahihi au uongofu wa Dini yake. Bila ya kujali rangi, mtazamo wa kisura, anavaa nini, kama ni tajiri au maskini, anatoka wapi, au pengine ukachukia kila kitu chake ila ukampenda kwa ajili ya Imani yake: Huku ndiko kupendana kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).


“Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema katika Hadiyth Al-Qudsiy: Wale ambao wana upendo wa dhati kwa ajili ya Utukufu Wangu watakuwa na nguzo ya mwangaza, watahusudiwa na Mitume na mashahidi.” [At-Tirmidhiy na Musnad Ahman]

SubhanAllaah! Fikiria kuhusudiwa na Mitume aliowachagua Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) mwenyewe, na wale waliofariki kwa ajili ya njia na radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)!. Hayo ni malipo makubwa sana kwa wale wanaopendana kwa ajili ya Mola wao Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).


  1. “Mwanaume anayeitwa na mwanamke mrembo kwa kutaka kufanya matendo ya haramu na akasema “La hakika mimi namuogopa Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala)…” Dunia hii imejaa vishawishi ambavyo vinaelekeza kwenye moto wa jahannam na miongoni mwa hivyo vishawishi ni vile vinavotokana na wanawake. Wanaume wengi wameelekeza mioyo na nafsi zao kwenye maangamizi ya vishawishi vya wanawake na pia ndio maana Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatuonya Ummah wake mahsusi kuhusu suala hili. Akasema, “Dunia ni nzuri na ya kijani na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atakuwekeni na Atakufanyeni nyinyi kuwa mlioendelea ili Aone mutakayoyatenda. Basi Jiepusheni na ushawishi unaotokana na wanawake: Hakika mtihani wa mwanzo wa wana wa Israaiyl ulisababishwa na wanawake.” [Muslim]

Ni muhimu sana kujiandaa na kujikinga kutokana na fitnah hii inayosababishwa na wanawake na vishawishi vengine vyote katika maisha kwa kumhofu Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).  Jambo hili hakika pia limezungumziwa katika Aayah ya Qur-aan ifuatayo: “Na ama yule anayeogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio, Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake!.” [An- Naazi`aat: 40-41].
  1. “Mtu anayetoa sadaka kwa mkono wa kulia na wa kushoto usijue kitu kilichotendeka (atoae sadaka kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa siri bila ya wengine kujua … Hii inaeleza aina ya mtu anayeelekea katika umbali wa hali ya juu kabisa katika kujilinda na kujiepusha na Riyaa (kufanya amali njema ili watu wamuone na kumsifu). Dhambi hii kubwa inaangamiza faida ambazo zimo kwenye amali njema na husababisha adhabu kali kwa yule anayefanya jambo hilo. Ni hatari kwa kuwa ni tabia ya binaadamu kupenda na kufurahia watu wakimhimidi (wakimtukuza). Hivvo ni lazima tuwe makini sana na kuhakikisha kuwa nia zetu zinaanza na kuendelea kubakia kuwa safi kila mara tufanyapo amali njema kama kutoa sadaka. Sio kama tunavoona leo ambapo katika Misikiti yetu utakuta watu katika kipaza sauti na mabao ya matangazo yanayosema, ‘Fulani katoa kadhaa kumpa fulanikwa sababu kadhaa wa kadhaa! Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anaonya kwa kusema: “Enyi mlioamini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na maudhi, kama anayetoa mali yake kwa kuwaonyesha watu, wala hamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama mfano wa jabali ambalo juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa, ikaliacha tupu. Basi hawatakuwa na uweza wowote kwa walivyo chuma. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri… [al-Baqarah: 264]. Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) atukinge katika jambo hili na atuongoze katika njia za kheri!
  1. Mtu anayemkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa faragha na huku macho yake yakatokwa na machozi.” Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametueleza: Ingelikuwa unayajua ninayoyajua mimi, ungeli cheka kidogo na ukalia sana.” [Al-Bukhaariy]

Kulia machozi sio alama ya udhaifu. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye alikuwa ndio binaadamu bora kabisa kuliko viumbe vyote, alikuwa akilia na pia Maswahaba zake wakifanya hivyo hivyo. Machozi ni njia thabiti ya kuonesha uoga wetu juu ya adhabu kali za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), upendo wetu wa dhati na kweli juu yake na hayaa (fazaa) juu yake. Lakini je, ni mara ngapi tunamkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa faragha au upweke na huku machozi yakatutoka? Kiasi gani tunacheka na kufurahi kwa wingi na kulia kidogo sana? Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna kitu ambacho kinampendezesha na kupendwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kama matone mawili na alama mbili: Tone la chozi lilotoka kwa ajili ya kumwogopa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), na tone la damu lilitoka kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Na hizo alama mbili ni, alama iliyosababishwa kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), na alama iliyosababishwa kwa kutimiza moja kati ya mambo ya fardhi yaliyoamrishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)…” [At-Tirmidhiy na katika Mishkaat]

Alhamdulillaah, kwa mafunzo tunayoyapata kutokana na hawa watu wa aina saba (7) waliotajwa katika Hadiyth, tumepewa alama wazi wazi za kutuongoza katika kupata starehe na ridhaa au utoshelezi. Kwa hiyo, Ndugu zangu Waislamu tujitolee na tufanye jitihada kubwa ili tuwe  miongoni mwa hawa watu saba, kwa hakika watu wenye bahati watakuwa wale watakaopewa kivuli cha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) katika siku ambayo kutakuwa hakuna kivuli chochote isipokuwa cha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) pekee. Aamiyn
********************************************************************************

Zifunge Siku Sita Shawwaal

Naaswir Haamid

Mgeni wetu Ramadhaan ametuondoka tukiwa bado tunamuhitajia kwa hamu kubwa. Ametuachia mafunzo mengi mazuri na miongoni mwao ni funga ya Sita Shawwaal.
Hii ni funga ambayo ameihimiza mno Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pale aliposema:

((Mwenye kufunga Ramadhaan kisha akaifuatilizia siku sita katika mwezi wa Shawwaal (mfunguo mosi) inakuwa kama aliyefunga mwaka (mzima kamili).)) [Imepokewa na Imaam Muslim]

Basi ni nani ambaye hataki kupata fadhila za siku hizi sita tu? Iwapo Muislamu amefunga masiku yote ya Ramadhaan basi anashindwa kufunga siku hizi tu? Ni aibu kweli kweli, ni sawa na kusema: 'umekula ngo'mbe wote amekushinda mkia.'

Fadhila za Swawm ni nyingi mno haswa pale Muislamu anapofunga kwa ajili ya kupata radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Nayo ni ‘ibaadah pekee ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anaijua siri ya mja wake kinyume na Swalah ambayo tunaonana tukiswali.

Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametufundisha kwamba mwenye kufunga angalau siku moja basi Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atamuokoa mja huyo kutokana na adhabu za Moto kwa umbali wa miaka sabini:

Kutoka kwa Abu Sa’iyd Al Khudriyy (Radhiya Allahu ‘anhu) hakika Mtume (swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mwenye kufunga siku [moja] kwa ajili ya Allaah, [Allaah] Atamuokoa uso wake kutokana na moto kwa umbali wa miaka sabini.)) [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim].

Hizi ndizo ‘amali za kuzifanya kwa wakati huu tukiwa hai. Kwani Qiyaamah hakuna fedha, dhahabu, makasri wala chengine ambacho kitamfaa mwanadamu. Ni amali zake za khayr ndizo zitakuwa muombezi wake. Na funga ya Sunnah ya Sita Shawwaal itakuwa miongoni mwao.

Miongoni mwa maombezi ya Qiyaamah ni ‘amali za Swawm na Qur-aan. Mwenye kuvipuuza vitu hivi navyo vitampuuza siku ya Hisabu. Itakuja Swawm siku ya Hisabu ikimuombea mja kwamba alikuwa akiacha kinywaji chake na chakula chake kwa ajili ya kupata radhi za Muumba. Naye kwa Rahmah Zake Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atampatia shafa’ah mja Wake. Hii sio siku ya kutegemea uombezi kutoka kwa baba, mama, ndugu wala rafiki. Hao sio kabisa! Zaidi labda wakuangamize kwa kudai haki zao juu yako wakufanye muflis wa ‘amali zako njema.

----------------------------------------------------****************----------------------------------
Laylatul-Qadr- Vipi Uweze Kuupata Usiku Huu?
Tumeingia   kumi la mwisho, kumi ambalo ndani yake kuna siku tukufu, siku ya Laylatul-Qadr, ambayo ibada yake ni bora kuliko ibada ya miezi elfu.
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):  
﴿ بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ﴾
((إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ)) (( وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ)) (( لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ))  ((تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ)) ((سَلَامٌ هِيَ حَتَّى مَطْلَعِ الْفَجْرِ))
BismiLlaahir Rahmaanir Rahiym
((Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan katika Laylatul Qadr,  (Usiku wa Makadirio[Majaaliwa]). Na nini kitachokujuulisha nini Laylatul Qadr?)) ((Laylatul-Qadr ni bora kuliko miezi elfu)) ((Huteremka Malaika na Roho (Jibriyl) katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao kwa kila jambo)) ((Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri))  [Al-Qadr: 1-5]

Vile vile dalili katika Hadiyth mbali mbali zimethibiti kuhusu Fadhila za usiku huu mtukufu, na jinsi Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyokuwa hali yake katika siku hizi kumi za mwisho za Ramadhaan.
Baada ya kuzijua fadhila zake usiku huu mtukufu inakupasa Muislamu ujikaze katika siku kumi hizi za mwisho kuacha mambo yote yanayokushughulisha ya dunia na utumbukie katika ibada tu ili uweze kuupata usiku huo mtukufu, yaani ukukute wewe ukiwa katika ibada ili zihesabiwe ibada zako kama kwamba umefanya ibada ya miezi elfu.

Tukifanya hesabu miezi elfu hiyo ni sawa na umri wa miaka 83!  
1000 ÷ 12 = 83.3 yaani miaka themanini na tatu na miezi mitatu takriban.
Hivyo ikiwa Laylatul-Qadr imekukuta katika ibada ya aina yoyote, ikiwa ni Swalah (Qiyaamul-Layl), kusoma Qur-aan, kufanya aina za dhikr, kutoa sadaka, kulisha chakula, kuwasiliana na jamaa, kujielimisha au kuelimisha, kufanya wema kwa watu, yote hayo utaandikiwa kama umefanya hayo kwa umri wa miaka 83! Na juu ya hivyo ibada hiyo ya usiku mmoja tu ni bora zaidi kuliko ibada utakayoweza kufanya miaka 83 na miezi mitatu. Subhaana Allaah!
Jihadhari ndugu Muislamu usije ukakukuta usiku huu mtukufu ukiwa katika maasi au katika sehemu ukiwa  umeghafilika na ya dunia kama sokoni, magenge ya soga au michezo ya kupoteza wakati au kwenye televisheni ukiangalia misalsalaat, mipira na sinema zikakupita kheri zote za usiku huu. Utaona siku hizi Waislamu wengi wanashughulika kwenda madukani kutafuta nguo za 'Iyd khaswa kina dada wakiacha masiku haya yawapite wakiwa humo badala ya kuwa majumbani mwao au misikitini kufanya ibada na kutegemea kuupata usiku huu.   
Ni siku chache tu ndugu Waislamu ambazo zinakimbia kama upepo. Je, nani basi katika sisi atakayepuuza asiupate usiku huo? Na Nani katika sisi atafanya hima kuupata usiku huo? Kwani hatujui kama tutakuweko duniani mwakani kuzipata siku hizi au hata hatujui kama tutaikamilisha Ramadhaan hii. Basi tujitahidi kwa kukesha  siku kumi hizi na kuamsha familia zetu ili iwe kheri yetu kukutana na usiku huo mtukufu tuweze kupata fadhila zake hizo ambazo ni sawa na kulipwa malipo ya umri mrefu kama tulivyoona hapo nyuma hata kama hatutoruzukiwa umri huo.

Mwenye Kuukosa Usiku Huu Amekula Khasara Kubwa
Hakika mwenye kuukosa usiku huo atakuwa amenyimwa kheri zake na itakuwa ni khasara kuukosa usiku huu mtukufu kama anavyosema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):   
عَنْ أَبِي هُرَيْرَة رَضِيَ اللَّه عَنْهُ قَالَ : لَمَّا حَضَرَ رَمَضَان قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: (( قَدْ جَاءَكُمْ شَهْرُ رَمَضَان شَهْرٌ مُبَارَكٌ اِفْتَرَضَ اللَّهُ عَلَيْكُمْ صِيَامَهُ تُفْتَح فِيهِ أَبْوَاب الْجَنَّة وَتُغْلَق فِيهِ أَبْوَابُ الْجَحِيم وَتُغَلُّ فِيهِ الشَّيَاطِين فِيهِ لَيْلَة خَيْرٌ مِنْ أَلْف شَهْر مَنْ حَرُمَ خَيْرهَا فَقَدْ حُرِمَ)) رَوَاهُ النَّسَائِيّ
Kutoka kwa Abu Huraryah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba ilipofika Ramadhaan, amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Umekujieni mwezi wa Ramadhaan, ni mwezi wa Baraka. Imefanywa Swawm kwenu kuwa ni Fardh, milango ya Pepo hufunguliwa na milango ya moto hufungwa na mashaytwaan hufungwa. Umo katika mwezi huu usiku ulio bora kuliko miezi elfu.  Atakayenyimwa kheri zake hakika kanyimwa haswa)) [An-Nasaaiy]

Siku hiyo ni siku iliyoteremeshwa Qur-aan kutoka mbingu ya saba hadi mbingu ya kwanza kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala):
﴿ بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ﴾
((حم)) ((وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ))  (( إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ))  ((فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ))   
BismiLlaahir Rahmaanir Rahiym
((Haa Miym)) ((Naapa kwa Kitabu kinachobainisha)) ((Hakika Tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji)) ((Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima)) [Ad-Dukhaan: 1-4]

Aya ya nne inayosema 'Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikma' kuwa kuna makadirio ya mwaka huo na yote yatakayotokea katika mwaka mzima. Kwa maana kwamba, siku ya Laylatul-Qadr, makadirio yote yaliyomo katika Al-Lawhum-Mahfuudhw (Ubao uliohifadhiwa) na huteremshwa haya makadirio na Malaika ambao wanaandika makadirio ya mwaka unaokuja yakiwa ni kuhusu umri wetu wa kuishi, rizki zetu, na yatakayotokea yote hadi mwisho wake. [Imesimuliwa na Ibn 'Umar, Mujaahid, Abu Maalik, Adh-Dhwahaak na wengineo katika Salaf – Ibn Kathiyr: 8:671]
Kujikaza kufanya ibada
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa inapoingia kumi la mwisho akijikaza kwa kufanya ibada kuliko siku zozote zingine:
عن عائشة رضي الله عنها قالت: كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يجتهد في العشر الأواخر ما لا يجتهد في غيره.  رواه مسلم

Kutoka kwa Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba: "Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akijitahidi katika kumi la mwisho kuliko alivyojitahidi katika siku nyingine zozote" [Muslim]

Na katika Swahiyhayn (Al-Bukhaariy na Muslim):  
عن عائشة رضي الله عنها، قالت: "كان رسول الله صلى الله عليه وسلّم إذادخل العشر شذ مئزره، وأحيا ليله، وأيقظ أهله  ( وفي رواية) "أحيا الليل،وأيقظ أهله، وجدّ، وشدّ المئزر" رواه البخاري ومسلم
Kutoka kwake pia Mama wa Waumini  'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha):  "Ilipokuwa inaingia kumi (la mwisho) Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikaza izaar (shuka) yake, akikesha usiku, na akiamsha ahli zake" (Na katika riwaaya nyingine) "Akikesha usiku, akiamsha ahli zake, akijitahidi na akikaza izaar yake" [Al-Bukhaariy na Muslim]

Kwa Nini Umeitwa Laylatul-Qadr?

Amesema Shaykh Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Llaah):

Kwanza: Kutokana na uwezo nao ni utukufu kama vile kusema “fulani mwenye uwezo mkubwa" yaani mwenye hadhi au utukufu.   

Pili: Ni usiku ambao una makadirio ya mwaka mzima na huandikwa yote yatakayotokea mwaka huo, na hii ni Hikma ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) na kuonyesha usanifu wa utengenezaji Wake na Uumbaji Wake.  

Tatu: Usiku huo una uwezo mkubwa kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):  
من قام ليلة القدر إيمانا واحتسابا غفر له ما تقدم من ذنبه)) متفق عليه

((Atakayesimama  usiku wa Laylatul-Qadr kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) [Al-Bukhaariy na Muslim]  
  
Sababu Ya Kupewa Waislamu Laylatul-Qadr
Sababu ya kupewa Ummah huu wetu wa Kiislamu siku hii tukufu ya Laylatul-Qadr ni kwamba:

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliona umri wa Ummah za mwanzo ni mrefu, na umri wa Ummah wake ni mfupi akapewa usiku wa Laylatul-Qadr uwe ni bora kuliko miezi elfu. [Muwatwtwaa 1/321 (Muhammad Fuad 'Abdul-Baaqy]

Ibada Za Kufanya Masiku Kumi Haya Katika Kukesha

1-Qiyaamul-Layl (Kisimamo cha usiku kuswali)
((من قام رمضان إيماناً واحتساباً غفر له ما تقدم من ذنبه)) متفق عليه
((Atakayesimama (Kuswali) Ramadhaan kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

2-Kuosma Qur-aan
Khaswa kwa vile usiku wa Laylatul-Qadr ndio usiku ulioteremeshwa Qur-aan kama tulivyoona katika Aayah hizo za juu katika Suratul-Qadr na Suratud-Dukhaan.
Vile vile Ramadhaan nzima inampasa Muislamu asome Qur-aan kwani ni mwezi ulioteremshwa Qur-aan kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
((شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ))
((Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi)) [Al-Baqarah: 185]

Na Jibriyl ('Alayhis-Salaam) alikuwa akimteremkia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kila usiku wa Ramadhaan akimsomesha na kumsikiliza Qur-aan:
"كَانَ رَسُولُ اللَّهِ -صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ- أَجْوَدَ النَّاسِ وَكَانَ أَجْوَدُ مَا يَكُونُ فِي رَمَضَانَ حِينَ يَلْقَاهُ جِبْرِيلُ وَكَانَ يَلْقَاهُ فِي كُلِّ لَيْلَةٍ مِنْ رَمَضَانَ فَيُدَارِسُهُ الْقُرْآنَ"-  رواه البخاري
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ni  mbora (mwenye matendo mema) wa watu, na alikuwa mbora zaidi katika Ramadhaan kwa sababu Jibriyl alikuwa akimjia kila usiku wa Ramadhaan akimfundisha Qur-aan)) [Al-Bukhaariy]

3- I'tikaaf
Kutia nia kubakia msikitini kwa kufanya ibada tu humo kwani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya hivyo:
 عن عائشة – رضي الله عنها- قالت "كان النبي يعتكف في كل رمضان عشرة أيام؛ فلما كان العام الذي قبض فيه اعتكف عشرين يوماً - أخرجه البخاري    
Kutoka kwa Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba: Mtume (swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya I'tikaaf kila Ramadhaan siku kumi, ulipofika mwaka wake wa kuaga dunia alifanya I'tikaaf siku ishirini" [Al-Bukhaariy]

4-Kuomba Maghfirah
Kwani usipoghufuriwa madhambi yako basi ni hatari!
عَنْ أَنَس وَغَيْره أَنَّ النَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمَّا صَعِدَ الْمِنْبَر ثُمَّ قَالَ  (( آمِينَ آمِينَ آمِينَ)) " قِيلَ يَا رَسُول اللَّه عَلَامَ مَا أَمَّنْت ؟
 قَالَ (( أَتَانِي جِبْرِيل فَقَالَ يَا مُحَمَّد رَغِمَ أَنْف رَجُل ذُكِرْت عِنْده فَلَمْ يُصَلِّ عَلَيْك قُلْ آمِينَ فَقُلْت آمِينَ ثُمَّ قَالَ رَغِمَ أَنْف رَجُل دَخَلَ عَلَيْهِ شَهْر رَمَضَان ثُمَّ خَرَجَ فَلَمْ يُغْفَر لَهُ قُلْ آمِينَ فَقُلْت آمِينَ ثُمَّ قَالَ رَغِمَ أَنْف رَجُل أَدْرَكَ وَالِدَيْهِ أَوْ أَحَدهمَا فَلَمْ يُدْخِلَاهُ الْجَنَّة قُلْ آمِينَ فَقُلْت آمِينَ)) صحيح الترمذي وقال الشيخ الألباني حسن صحيح  

Kutoka kwa Anas na wengineo kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipopanda juu ya minbar aliitikia ((Aamiyn, Aamiyn, Aamiyn)). Alipoulizwa kwa nini ameitikia hivyo akasema: ((Amenijia Jibriyl akasema: Ee Muhammad, ole wake yule ambaye unapotajwa hakuswalii, hivyo sema Aamiyn. Nikasema Aamiyn. Kisha akasema: ole wake yule ambaye umeingia mwezi wa Ramadhaan kisha akatoka bila ya kughufuriwa, kwa hiyo sema Aamiyn. Nikasema Aamiyn. Kisha akasema: ole wake yule ambaye amewakuta wazazi wake au mmoja wa wazazi wake lakini wasimuingize Peponi. Hivyo sema Aamiyn. Nikasema Aamiyn)) [Swahiyh At-Tirmidhiy na kasema Shaykh Al-Albaaniy kuwa Hadiyth hiyo ina daraja ya Hasan Swahiyh]

5-Du'aa Ya Kuomba Maghfirah Katika Siku Kumi Hizi Zakaatul-Fitwr Mwisho

عن عائشة رضي الله عنها أنها قالت يا رسول الله أرأيت إن وافقت ليلة القدر ما أدعو قال: ((تقولين: اَللَّهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌ تُحِبُّ الْعَفْو فَاعْفُ عَنِّي)) ابن ماجه و صححه الألباني
Kutoka kwa mama wa waumini bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba alisema "Ewe Mjumbe wa Allaah je, nitakapowafikiswha  usiku wa Laylatul-Qadr  niombe nini?" Akasema, ((Sema: Ewe Allaah Hakika Wewe Ndiye Mwenye Kusamehe Unapenda Kusamehe basi Nisamehe)) [Ibn Maajah na kaisahihisha Al-Albaaniy]  

Matamshi Yake
Allaahumma Innaka 'Afuwwun Tuhibbul-'Afwa Fa'afu 'Anniy

6-Kumkumbuka Allaah Kwa Aina Zozote Za Dhikr

Kwa Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl, Takbiyr (kusema: Subhaana Allaah, Alhamdulillah,  Laa Ilaaha Illa Allaah,  Allaahu Akbar)

7- Kuomba Du'aa Na Haja Zako
Kwa vile ni mwezi wa kuomba Du'aa pia kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala Ameunganisha Aayah za kufaridhishwa Swawm na Aaya za kuhusu kuomba Du'aa:
((وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ فَلْيَسْتَجِيبُواْ لِي وَلْيُؤْمِنُواْ بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ))  
((Na waja Wangu watakapokuuliza khabari Zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka)) [Al-Baqarah: 186]

Usiku Gani Khaswa Unapatikana Laylatul-Qadr? 
Hadiyth zimetaja siku kadhaa ambazo usiku huu mtukufu hutokea katika siku kumi za mwisho na haswa katika usiku wa witiri, zikiwa zimetajwa nyingine kuwa ni usiku wa siku ya ishirini na moja, au ishirni na tatu, au ishirni na tano au ishirini na saba kama ilivyokuja katika dalili zifuatazo:
وفي حديث عائشة رضي الله عنها أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((تحروا ليلة القدر في الوتر من العشر الأواخر)) رواه البخاري
Hadiyth kutoka Mama wa Waumini 'Aiashah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Utafuteni usiku wa Laylatul-Qadr katika siku za witiri kwenye siku kumi za mwisho)) [Al-Bukhaariy]

وفي حديث ابن عباس رضي الله عنهما أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((التمسوها في العشر الأواخر من رمضان ليلة القدر في تاسعة تبقى ، في سابعة تبقى ، في خامسة تبقى)) رواه البخاري

Hadiyth kutoka Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Utafuteni usiku wa Laylatul-Qadr katika siku kumi za mwisho za Ramadhaan, katika (usiku wa) tisa, saba, na wa tano utakaobakia [mwisho wa Ramadhaan])) [Al-Bukhaariy]
Imaam Ahmad amerikodi kutoka kwa 'Ubaydah bin Asw-Swaamit kwamba alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu usiku wa Laylatul-Qadr akasema: 
((فِي رَمَضَان فَالْتَمِسُوهَا فِي الْعَشْر الْأَوَاخِر فَإِنَّهَا فِي وِتْر إِحْدَى وَعِشْرِينَ أَوْ ثَلَاث وَعِشْرِينَ أَوْ خَمْس وَعِشْرِينَ أَوْ سَبْع وَعِشْرِينَ أَوْ تِسْع وَعِشْرِينَ أَوْ فِي آخِر لَيْلَة))
((Katika Ramadhaan, utafuteni siku kumi za mwisho, hakika umo katika siku za witiri, siku ya ishirini na moja, au ishirini na tatu, au ishirini na tano, au ishirini na saba, au ishirini na tisa, au usiku wa mwisho)) [Ahmad]

Alama Zinazobainisha Laylatul-Qadr
  1. Kwenye usiku huo kunakuwa na mwanga zaidi. 
  2. Upepo siku hiyo hutulia, yaani siku hiyo hautokei upepo mkali.
  3. Hali ya hewa huwa nzuri.
  4. Nyoyo siku hizo huwa na utulivu na unyenyekevu zaidi kuliko siku nyingine.
  5. Baadhi ya watu wema huoteshwa usiku kama walivyokuwa wakioteshwa Maswahaba na Salafus-Swaalih (wema waliotangulia) 


Asubuhi Yake
حديث أبي بن كعب رضي الله عنه أنه قال: "أخبرنا رسول الله صلى الله عليه وسلم أنها تطلع يومئذ ٍ لا شعاع لها" رواه مسلم
Hadiyth kutoka kwa Ubay bin Ka'ab (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba: "Ametuambia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa jua hutoka siku hiyo likiwa halina mishale (mikali)" [Muslim]

(( ليلة القدر ليلة طلقة  لا حارة ولا باردة ، تُصبح الشمس يومها حمراء ضعيفة)) صحيح ابن خزيمة
((Laylatul-Qadr usiku ulio katika hali ya ukunjufu, usio na baridi wala joto, asubuhi yake jua huwa jekundu na dhaifu)) [Swahiyh Ibn Khuzaymah]

ليلة القدر ليلة بلجة  (أي مضيئة) لا حارة ولا باردة ، لا يرمى فيها بنجم))  (أي لا ترسل فيها الشهب) رواه الطبراني  ومسند أحمد
((Laylatul-Qadr usiku wa kung'aa [yaani wenye mwanga] sio joto wala baridi, na vimondo (nyota za kufyatuliwa) hazitotumwa)) [At-Twabaraaniy na Ahmad] 

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atuwezeshe kukesha masiku haya kumi ili tujaaliwe kuupata usiku huu mtukufu tutoke katika Ramadhaan hii tukiwa tumeghufuriwa madhambi yetu yote na tumepewa fadhila za usiku huu mtukufu zinazolingana na kuongezewa umri wa miaka 83.  Aamiyn



***********************************************************************************

Madhara Ya Ghiybah (Kusengenya) 2-Ulimi Ni Kufaulu Kwako Au Kuangamia Kwako


Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ameuhifadhi Ulimi ndani ya mdomo, ili usiwe wazi kila mara ukanena maneno mengi ambayo huenda yakamuangamiza binaadamu kwa kumuharibia amali zake, au kukosa radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). japo kwa neno moja tu ovu kama anavyosema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
عن أبي عبد الرحمن بلال بن الحارث المزني رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال‏:‏ ((‏إن الرجل ليتكلم بالكلمة من رضوان الله تعالى ما كان يظن أن تبلغ ما بلغت يكتب الله له بها رضوانه إلى يوم يلقاه، وإن الرجل ليتكلم بالكلمة من سخط الله ما كان يظن أن تبلغ ما بلغت يكتب الله له بها سخطه إلى يوم يلقاه))‏.‏ رواه مالك في الموطأ والترمذي وقال حديث حسن صحيح‏ 
Abu 'Abdir-Rahmaan Bilaal bin Al-Haarith Al-Muzniy (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kwa hakika mja atazungumza neno linalomridhisha Allaah, wala asidhani kuwa litafikia lilipofikia, Allaah Amuandikie kwa neno hilo Radhi Zake hadi Siku ya Qiyaamah. Na Kwa hakika mja atazungumza neno linalomkasirisha Allaah, wala asidhani kuwa litafikia lilipofikia, Allaah Amuandikie kwa neno hilo hasira Zake hadi Siku ya Qiyaamah)) [Maalik katika Muwattwa na At-Tirmidhiy ambaye amesema Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]
Kutokana na Hadiyth hii, tunapata funzo kwamba, ulimi unaweza kuwa ni kiungo kizuri kabisa katika mwili wa binaadamu na unaweza kuwa ni kiungo kiovu kabisa vile vile.
Kisa kifuatacho cha Mzee Luqmaan kinatuthibitishia funzo hili:
Ibn Jariyr amenukuu kwamba Khaalid ar-Rabaai alisema: "Luqmaan alikuwa mtumwa wa Kiethiopia aliyekuwa na ujuzi wa useremala. Bwana (Tajiri) wake alimwambia: "Tuchinjie kondoo huyu" Akamchinja, kisha akamwambia: "Niletee viungo viwili vilivyokuwa ni bora kabisa". Akampelekea ulimi na moyo. Baada ya siku kupita, alimtaka tena amchinjie kondoo, akachinja kisha Bwana wake akamwambia tena: "Niletee viungo viwili vilivyokuwa ni viovu kabisa". Akameletea vile vile ulimi na moyo. Bwana wake akamuuliza: "Nilipokutaka uniletee viungo bora kabisa umeniletea ulimi na moyo; na nilipokutaka uniletee viungo viovu kabisa umeniletea hivyo hivyo" Luqmaan akamwambia: "Hakuna vilivyo bora kuliko hivi vinapokuwa vizuri, na hakuna vilivyo viovu kabisa kuliko hivi vinapokuwa vibaya" [At-Twabariy: 20:135]
Mafunzo mengineyo kuhusu ulimi:
·         Ulimi ni kipande kidogo cha nyama kisichokuwa na mifupa lakini kinaweza kumvunja mtu mifupa yake siku ya Qiyaamah.
·         Ulimi ni kama nyoka itakayomtia sumu binaadamu, au ni kama mkuki utakaomuangamiza binaadamu siku ya Qiyaamah
·         Hivyo hivyo, ulimi huenda ukawa ni sababu ya kumuingiza mtu Peponi japo kama hakuwa na vitendo vyema vingi.


·         Ulimi ni kiungo kikuu katika mwili wa binaadamu kinachodhibiti viungo vingine vyote vya mwili wa binaadamu.




عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَفَعَهُ قَالَ : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:  (( إِذَا أَصْبَحَ ابْنُ آدَمَ ، فَإِنَّ الْأَعْضَاءَ كُلَّهَا تُكَفِّرُ  اللِّسَانَ ، فَتَقُولُ : اتَّقِ اللَّهَ فِينَا ، فَإِنَّمَا نَحْنُ بِكَ ، فَإِنِ اسْتَقَمْتَ اسْتَقَمْنَا ، وَإِنِ اعْوَجَجْتَ اعْوَجَجْنَا))  أخرجه الترمذي وأحمد وابن خزيمة والبيهقي بسند حسن. رياض الصالحي
Kutoka kwa Abu Sa'iydil-Khudriyy (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Anapoamka binaadamu viungo vyote vinaulaumu Ulimi vikisema: Mche Allaah kwetu, kwani sisi tuko katika hifadhi yako; ukiimarika nasi tutaimarika, ukienda pogo, nasi tutakwenda pogo)) [At-Tirmidhiy, Ahmad, Ibn Khuzaymah, Al-Bayhaqiy ikiwa ni sanad hasan. Riyaadhwus-Swaalihiyn]
Ni vyema  kuzuia ulimi usitoke tu kuzungumza maneno yoyote ila kwa kuhitajika, kwani kuuachia ulimi mradi tu uzungumze utampeleka mtu kutoa porojo na kuzungumza yasiyofaa na kumharibia mja Akhera yake.


*****************************************************************************

Qiyaamul-Layl - 1 (Fadhila Za Kusimama Kuswali Usiku)




Amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



((من قام رمضان إيماناً واحتساباً غفر له ما تقدم من ذنبه))  متفق عليه



((Atakayesimama (Kuswali) Ramadhaan kwa imaani na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) [Al-Bukhaariy na Muslim]



Amesema Al-Haafidh ibn Rajab, "Tambua kuwa Muumini anajumuisha katika mwezi wa Ramadhaan jihaad mbili kwa ajili ya nafsi yake.  Jihaad ya mchana ya kufunga, na jihaad ya usiku kwa kusimama (kuswali), atakayejumuisha jihaad hizi mbili atapata ujira wake bila ya hesabu".



Amesema Ibn 'Uthaymiyn "Haimpasi Muislamu kuepukana na Swalah ya Tarawiyh katika Ramadhaan ili apate thawabu na ujira wake, na wala asiondoke mpaka Imaam amalize pamoja na Swalah ya Witr ili apate ujira wa Qiyaamul-Layl yote".



Ili kuipata ladha ya Ramadhaan na kuongeza Utiifu na Imaan ni muhimu Muislamu ajumuike na Waislamu wenzie kuswali Tarawiyh na kusikiliza Tilaawat ya Qur'aan inaposomwa katika Swalah hizi kupata utulivu wa moyo na nafsi na pia kujichumia thawabu tukufu zinazopatikana katika kisimamo hiki na kufutiwa madhambi yake kama tulivyoona kwenye hadiyth iliyopita.



KWA NINI MUISLAM ASWALI QIYAAMUL-LAYL?



Zifuatazo ni sababu ambazo zinampasa Muislamu azizingatie na afanye hima kuswali Swalah ya Qiyaamul-layl ili aweze kupata fadhila njema za kumfanya awe Muumini bora kabisa:



1-QIYAAMUL-LAYL NI AMRI KUTOKA KWA ALLAAH (Subhaanahu wa Ta'ala) 



}}يآ أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ{{  }} قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا{{  }} نِصْفَهُ أَوِ انقُصْ مِنْهُ قَلِيلًا{{   }} أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا {{



{{Ewe uliyejifunika}} {{Kesha usiku kucha, ila kidogo tu!}} {{Nusu yake, au ipunguze kidogo}} {{Au izidishe - na soma Qur-aan kwa utaratibu na utungo}}[Al-Muzammil: 1-4]



}}أَقِمِ الصَّلاَةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَى غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا{{

 }} وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَى أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا{{

{{Shika Swalah jua linapopinduka mpaka giza la usiku, na Qur'ani ya alfajiri. Hakika Qu-aan ya alfajiri inashuhudiwa daima}}

{{Na amka usiku kwa ibada; ni ziada ya Sunnah khasa kwako wewe. Huenda Mola wako Mlezi Akakunyanyua cheo kinachosifika}} [Al-Israa 78-79]
 
Tahajjud ni Swalah inayoswalia baada ya kulala, tunaona katika Hadiyth mbalimbali kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  alikuwa akiswali Tahajjud baada ya kulala. Nazo ni kutoka kwa Ibn Abbaas na 'Aishah. Taz.Fathul Baari 8.83 ,  3:39



Amesema  Mujaahid, "Qiyaam kwa haki ya Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni Naafilah (Ziada ya Sunnah) kwa sababu ameshafutiwa madhambi yake yaliotangulia na yaliyokuja.  Na kwa haki ya Umma wa Kiislamu Swalah ya  Qiyaamul-Layl huenda ikamfutia madhambi yake atakayotenda".  [At-Twabariy 17:525]



Na Amesema tena Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)    



}}فَاصْبِرْ عَلَى مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ الْغُرُوبِ{{

}}وَمِنَ اللَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَأَدْبَارَ السُّجُودِ{{



{{Basi vumilia kwa hayo wasemayo, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa}} 

{{Na katika usiku pia mtakase, na baada ya kusujudu}}. [Qaaf:39-40]

Amesema tena:

}}وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا{{

 }} وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَهُ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا{{



{{Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni}}

{{Na usiku msujudie Yeye, na umtakase usiku, wakati  mrefu}}[Al-Insaan:25-26]



 2- KUMSHUKURU ALLAAH (Subhanaahu wa Ta'ala) 

     

Qiyaamul-Layl ni mojawapo ya njia ya kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  kwani kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  sio kwa kusema tu bali iwe shukurani ndani ya moyo na kukiri kwa ulimi na kwa viungo pia kama alivyokuwa akifanya Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

    

وعن عائشة رضي الله عنها قالت )) كان النبي يقوم من الليل حتى تتفطر قدماه. فقلت له: لِمَ تصنع هذا يا رسول الله،   وقد غُفر لك ما تقدم من ذنبك وما تأخر؟ قال: أفلا أكون عبداً شكوراً ؟ ((متفق عليه




 

((Imetoka kwa Bibi 'Aaishah (Radhiya Allahu 'anha) kwamba Mtume   alikuwa akisimama usiku hadi ikivimba miguu yake, nikamwambia  kwa nini unafanya hivi ewe Mjumbe wa  Allaah, na hali umefutiwa madhambi yako yaliyotangulia na yatakayofuatia?  Akasema, "Nisiwe mja mwenye kushukuru?))  [Al-Bukhaariy na Muslim]

3- SWALAH BORA KABISA BAADA YA FARDH



         Amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  



((أفضل الصلاة بعد الفريضة صلاة الليل))  رواه مسلم.



((Swalah iliyo  bora kabisa baada ya Fardh ni Swalah ya usiku))  [Muslim]
 
4- KUFUFUA NA KUFUATA SUNNAH YA MTUME (Swalla Allahu 'alayhi wa alihi wa sallam)   NA MASWAHABA ZAKE

Badala ya kukesha usiku kwa mambo mengine ya kidunia yasiyo na  faida na sisi wala Akhera yetu na kupoteza umri wetu, ni bora kukesha kwa kumuelekea Mola Mtukufu kwa kufuata Sunnah za kipenzi chetu Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  na Maswahaba zake



5- KUBADLISHA HALI ZIWE KAMA ZA SALAF SWAALIH (WEMA WALIOPITA)  





Ni mwendo wa Salaf Swaalih ambao uliendelea  hadi kutufikia sisi adabu ya kutekeleza Swalah hii ambayo ni mojawapo wa nyenzo bora kabisa kuzidisha imani zetu, kusafisha nyoyo zetu, kupata utulivu  na kupata Ridhaa ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) 









6- KUJIKURUBISHA NA ALLAH  (Subhanaahu wa Ta'ala)





((وعن عمرو بن عبسة رضي الله عنه أنه سمع النبي  صلى الله عليه وسلم  يقول: أقرب ما يكون الرب من العبد   في جوف الليل الآخر فإن استطعت أن تكون ممن يذكر الله تعالى  في تلك الساعة فك))رواه الترمذي وأبو داود


((Imetoka kwa 'Amru bin 'Abasah (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba kamsikia Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)    akisema: ((Wakati Allaah Anakuwa karibu kabisa na mja, ni wakati wa mwisho wa usiku, kwa hiyo ukiweza kuwa miongoni mwa wanaomkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)   katika saa hiyo basi uwe)) [At-Tirmidhy na Abu Dawuud].  



   

7- KUJIKINGA NA UCHAFU WA SHAYTWAAN





ذكر عند النبي رجل نام ليلة حتى أصبح فقال:  ))ذاك رجل بال الشيطان في أذنيه    ((متفق عليه





Alielezwa Nabii kuwa kuna mtu alilala usiku wote hadi asubuhi bila kuswali, Akasema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((huyo ni mtu aliyekojolewa na Shaytwaan katika masikio yake)) [Al-Bukhaariy na Muslim].

 





Inaendelea....../2




*****************************************************************

 Hadith no 2: Allaah Hupokea Toba Za Waja Usiku Na Mchana



عَنْ أَبِي مُوسَى عَبْدِ الله بنِ قَبَسٍ الأَشْعَرِيِّ  (رضي الله عنه) عن النَّبيّ (صلى الله عليه و آله وسلم) قال: ((إِنَّ اللَّهَ تَعَالَى يَبْسُطُ يَدَهُ بِاللَّيْلِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ النَّهَارِ وَيَبْسُطُ يَدَهُ بِالنَّهَارِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ اللَّيْلِ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَا)) رواه مسلم
Imepokewa kutoka kwa Abu Musaa ‘Abdillaah bin Qays Al-Ash‘ariyy (رضي الله عنه)  kwamba Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakika Allaah Anakunjua Mkono Wake usiku ili Apokee toba ya mkoseaji mchana. Na Anakunjua Mkono Wake mchana ili Apokee toba ya mkoseaji usiku mpaka jua lichomoze Magharibi)[1]

Faida ya Hadithi:

  1. Umuhimu wa mja kukimbilia kutubu anapofanya maasi mchana au usiku. [At-Tahriym 66: 8, An-Nuwr 24: 31].

وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ
Na kimbilieni maghfirah kutoka kwa Mola wenu na ili mpate pepo upana wake ni wa mbingu na ardhi imeandaliwa kwa wenye kumcha mungu[2]

  1. Rehma ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa waja Wake kuwapa muda wa kutubia maasi, lau sivyo Angeliwaadhibu na kuwaangamiza hapo hapo wanapotenda maasi. [Faatwir 35: 45, An-Nahl 16: 61].

  1. Rehma ya Allaah kwa waja Wake kutokutofautisha wakati wa Toba japokuwa maasi mengine yanazidi mengineyo. 

  1.  Toba inaendelea kupokewa hadi milango ifungwe: [Hadiyth: ((Hakika Allaah Huikubali Toba ya mja Wake kabla ya roho kufika kwenye mkoromo wa mauti)[3] ((Atakayetubu kabla ya kuchomoza jua upande wa Magharibi, Allaah Atamkubalia toba yake)).[4]

  1. Hii inaonyesha mahaba makubwa ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kuwapatia fursa hii ya dhahabu ambayo haifai kupotezwa na waja wenyewe.

  1. Hadithi inatoa mafunzo kwa Muislamu kuto kumuhukumu mwenziwe kuwa hatoghufuriwa madhambi yake. [Rejea Hadiyth namba 99].

  1. Mja hata afanye madhambi makubwa vipi, asikate tamaa na Rehma ya Allaah (سبحانه وتعالى), kwani Yeye Hughufuria madhambi yote. [Az-Zumar 39: 53]

[1]  Muslim.
[2]  Aal-‘Imraan (3: 133).
[3]  At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad, na imepewa daraja ya Swahiyh na Al-Albaaniy.
[4]  Muslim.

  ************************************************************

Hadith Ya 1 :Allaah Hatazami Miili Wala Sura za waja, Bali Anatazama Nyoyoni

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ  (صلى الله عليه و آله وسلم): ((إِنَّ اللَّهَ لاَ يَنْظُرُ إِلى أجْسَامِكُمْ  وَلاَ إِلَى صُوَرِكُمْ وَلَكِنْ يَنْظُرُ إِلَى قُلُوبِكُمْ)) رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakika Allaah Hatazami viwiliwili vyenu wala sura zenu, lakini Anatazama nyoyo zenu))[1]

Mafunzo Na Hidaaya:

  1. Umuhimu wa kuwa na NIA safi na ikhlaasw katika kumuabudu Allaah (سبحانه وتعالى) kwani hivyo ndivyo tulivyoamrishwa:

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ
 Na hawakuamrishwa ila kumwabudu Allaah kwa kumtakasia Dini, hunafaa [wakielemea Dini ya haki na kuacha Dini potofu] na wasimamishe Swalaah, na watoe Zakaah, na hiyo ndiyo Dini iliyo sawa[2]

  1. Hima ya kutenda ‘amali njema baada ya kuwa na  NIA safi.

  1. ‘Amali na ‘Ibada hazipokelewi isipokuwa NIA ikiwa ni safi kwa ajili ya Allaah (سبحانه وتعالى) [Al-Kahf 18: 103-104, 110, Al-Furqaan 25: 23].

  1. Hakuna ajuaye yaliyo moyoni mwa mja isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى) [Al-Mulk 67: 13, Huwd 11: 5, Faatwir 35: 38, Al-Hadiyd 57: 6, At-Taghaabun 64: 4].

يَعْلَمُ خَائِنَةَ الْأَعْيُنِ وَمَا تُخْفِي الصُّدُورُ
(([Allaah] Anajua hiyana ya macho na yanayoficha vifua))[3]

  1. Binaadamu hawezi kuficha kitu kwa Allaah, kwani ‘amali na siri zote zitadhihirika Siku ya Qiyaamah. [Aal-‘Imraan 3: 29, Az-Zumar 39: 7, Al-An’aam 6: 60, At-Tawbah: 94, Al-Jumu’ah 62: 8, Atw-Twaariq 86: 9].

  1. Ni muhimu kwa Muislamu kuzitekeleza amri za Dini yake na si kwa mandhari pekee. Na mara nyingi watu huwa ni wenye kusema pindi anapotenda jambo ovu kuwa: “Lakini NIA yangu ni nzuri”. Hapa Muislamu anatakiwa aizingatie Hadith nyengine inayosema: ((Hakika Allaah Hatazami viwiliwili vyenu wala sura zenu, lakini Anatazama nyoyo na ‘amali zenu)).[4] Hivyo, ‘amali zinafaa ziende sambamba na Aliyoyateremsha Allaah na kuja nayo Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).
  1. Usimhukumu mtu kwa mandhari yake, pindi ukimuona mtu umbile lake na hakuvaa mavazi ya Muumin ukadhania ni mtu muovu, huenda akawa ni mwema. Hali kadhalika, pindi ukimuona mtu umbile lake na mavazi yake ni ya ki-Muumin ukadhani kuwa ni mtu mwema kabisa, lakini huenda akawa ni mtu muovu.
  1. Kuzingatia yanayomridhisha Allaah (سبحانه وتعالى) daima.

  2. MAREJEO YA AYA NA HADITHI
[1]  Muslim.
[2]  Al-Bayyinah (98: 5).
[3]  Ghaafir (40: 19).
[4]  Muslim.

0 comments:

Post a Comment