Feb 16, 2015

JANUARY MAKAMBA AIJIA JUU MITANDAO YA SIMU KWA KUPANDISHA BANDLE

Naibu waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknoljia Mhe January Makamba,amesema haungi mkono kupanda kwa gharama za vifushi vilivyotangazwa hivi karibuni na makampuni ya simu.

Ameyasema hayo jana katika mahojiano maalumu yaliyofanyika baina yake na Munira Blog  muda mfupi baada ya kumalizika Mkutano Mkuu wa Umoja wa wakaazi wa mkoa wa Tanga waishio Dar es salaam (UMATADA) .

"Nimemuagiza Prof Nkoma ambaye ni Mkurugenzi wa Tume ya mawasiliano anifahamishe mambo matatu ya Msingi" ,Alisema.

Aliyataja mambo hayo kua ni,kwanza kuna ughafla katika upandishaji huu,pili kuna ukubwa zaidi ya asilimia mia nne na tatu upandishaji wao wa pamoja hasa katika kipindi hiki cha biashara ubia.

"Inanitia shaka kuona zama hizi za ushindani wa biashara huru,kisha leo kwa pamoja wapandishe gharama za vifurushi vya internet", alisema.

"Yawezekana kuna ukiukwaji wa kanuni, ninafuatilia kujuwa ukweli,lakini nina ahidi,ikabainika hivyo tutawachukulia hatua".mwisho wa kumnukuu.

kumekua na malalamiko kutoka kwa watumiaji wa Intrenet,tangu Makampuni ya Simu kupandisha gharama za vifurushi.

0 comments:

Post a Comment