Mar 18, 2016

TUPO IMARA; QIBLATAIN SCHOOL.


Wazazi na wadau wa elimu wametakiwa kuiamini na kuiunga mkono shule ya Qiblatai English Medium Primary School kutokana na hatua madhubuti iliyoichukua ya kuiimarisha shule hiyo.

Hayo yalisemwa jana na Mwalimu mkuu wa shule hiyo ndugu Shamsuddin Saleh wakati alipofanya mahojiano mafupi na munira blog muda mfupi baada ya kumalizika Bonanza hilo.

Amesema "shule yetu imejipanga vyema,ina walimu bora na wachapakazi chini ya Uongozi bora na imara,hali hii imeifanya shule yetu kuwa imara kinidhamu ni kitaaluma hivyo natoa wito kwa wazazi wawalete watoto wao ili tuwarithishe elimu bora yenye maadili mema".Alisema

Aliendelea kusema kwamba "hata bonanza hili, ni kielelzo kwamba shule ipo imara,kwani maandalizi yetu yalikuwa mazuri na makubwa kiasi kwamba ufanisi wake umedhihiri leo hii kiasi cha kuwafurahisha wazazi" mwisho wa kumnukuu.

Awali akiongea na waandishi wa habari,mwalimu wa taaluma Muhammada Muhiddiin alisema,michezo kwa watoto ni sehemu ya elimu,na michezo mbali ya kuimarisha afya ya mtoto lakini pia inakuza akili ya mtoto.

Qiblatain School ipo makutano ya mtaa wa Agrey na swahili kariakoo Jijini Dar es salaam.

Bonanza hilo lilifanyika jana katika viwanja vya Jakaya Kikwete vilivyopo kidongo chekundu Jijini Dar es salaa. 


Aidha hivi karibuni shule ya Qiblatain iliwatunuku zawadi ya pesa taslimu na vyeti kwa walimu wake waliofaulisha vyema mtihani wa mwaka jana 2015.


Baadhi ya washiriki wa bonanza hiyo wakijiandaa kupokea zawadi.



Mgeni rasmi Juma Rashid ( Mjumbe wa Bodi ya shule) akimkabidhi medali ya fedha mmoja wa wanafunzi washindi katika bonanza hilo,huku mwalimu mkuu shamsuddin (katikati) na mwalim Rajab Mgooh ( msalidizi mkuu wa taaluma) wakishuhudia tukio hilo. 
 Mmoja wa washindi akifurahi zawadi yake.
Mwalimu mkuu wa Qiblatain Shamsuddin Saleh ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi na pia mratibu wa bonanza hilo,wakati akifanya mahojiano mafupi na munira blog.

BAADHI AY MATUKIO YA KUKABIDHI ZAWADI YA PESA TASLIMU NA VYETI KWA WALIMU WALIOFAULISHA VIZURI KATIKA MTIHANI WA MWAKA 2015.



 MWALIMU RADHIA MWINYIMAD, AKIPOKEA ZAWADI YA PESA NA CHETI BAADA YA KUONGOZA KWA KUFAULISHA WANAFUNZI WENGI.
 MWALIMU MAKOYE ( MAARUFU KWA JINA LA MSUKUMA HALISI) AKIKABIDHIWA PESA TASLIMU BAADA YA KUFAULISHA.
 MWALIMU SONSO,AKIPOKEA ZAWADI YA PESA KUTOKA KWA ABDALLAH MBWANA AMBAYE NI KATIBU MSTAAFU WA BODI YA SHULE.


picha zote kwa hisani ya ALLY SHAABAN WA QIBLATAIN

1 comments:

  1. that is good as it encourage teachers towards hard working

    ReplyDelete