Gari zikiwaka moto baada ya shambulio dhidi ya kanisa katoliki la Madalla karibu na mji wa Abuja
Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Bindamu la Amnesty
Internationale linasema wanagambo wa kislamu wa Boko Haram nchini
Nigeria pamoja na jeshi la Nigeria wametekeleza kwa njia moja ima
nyingine uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Shirika hilo imeiomba Jumuiya ya Kimataifa kufanaya uchunguzi kuhusu visa vya ukiukwaji wa haki za Binadamu nchini Nigeria.Amnesty Internationale imetoa wito huo, baada ya kugundua kwamba watu 1500 waliuawa wakati machafuko yaliposhika kasi kaskazini mashariki mwa Nigeria kati ya jeshi na wanamgambo wa wa kiislamu tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Shirika hilo linasema kuwa ikiwa Jumuiya ya Kimataifa haitachukua hatua kuisaidia Nigeria hali huenda ikaendelea kuwa mbaya.
Taasisi inayo jihusisha na shughuli za uokozi nchini Nigeria NEMA ilibaini jumanne iliyopita kwamba kati ya watu zaidi ya 1000 wamepoteza maisha na wengine 250.000 waliyahama makaazi yao.
Kwa upande wake shirika linalotetea haki za binadamu la Human right Watch ilisema katika taarifa liliyotoa hivi karibuni kwamba watu 700 waliuawa tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Amnesty Internatinale, imesema kwamba nusu ya watu waliyouawa ni raia wa kawaida, huku ikibaini kwamba inatiwa hofu na ripoti zinazoonyesha kwamba watu takriban mia moja wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Boko Haramu waliuawa, baada ya uvamizi wa jela machi 14.
“Tunaomba Jumuiya ya Kimataifa kufanya uchunguzi wa haraka uliyo huru ili kuchunguza iwapo baadhi ya visa viliyotekelezwa havihusiane na uhalifu wa kivita au uhalifu dhidi ya binadamu”, amesema kiongozi wa ofisi ya utafiti katika bara la Afrika kutoka Amnesty, Netsanet Belay.
Shirika hilo limetolea wito Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika na Jumuia ya Uchumi ya Mataifa ya Magharibi CEDEAO), kutoa mchango wao ili kukomesha machafuko hayo yanayodumu tangu mwaka 2009, na kusababisha maelfu ya raia kuuawa.
0 comments:
Post a Comment