MUNIRA MADRASA & ISLAMIC PROPAGATION ASSOCIATION | |||||
ACCOUNTING FOR FINANCIAL AFFAIRS | |||||
AS AT : | 30-06-2013 | ||||
STRUCTURE | |||||
S/NO: | NATURE OF ASSETS / LIABILITY | QUANTITY | U/PRICE | VALUE | |
FIXED ASSETS | |||||
1 | BUILDING | 1 | 21,000,000.00 | ||
2 | FURNITURE | 26 | 635,000.00 | ||
3 | FITTINGS | 690,000.00 | |||
RADIO | 1 | 140,000.00 | |||
3 | MACHINES & EQUIPMENTS | 5,605,000.00 | |||
4 | LAND | 1 | 10,000,000.00 | ||
38,070,000.00 | |||||
CURRENT ASSETS | |||||
1 | CASH | 365,000.00 | |||
2 | STOCK | Books 400 | 1,500.00 | 600,000.00 | |
3 | DEBTORS | ||||
4 | PRE-PAYMENTS | ||||
965,000.00 | |||||
LIABILITIES | |||||
1 | CREDITORS | 492,000.00 | |||
2 | LOANS | ||||
3 | DUE PAYMENTS | ||||
WORKING CAPITAL | 473,000.00 | ||||
NET EQUITY | 38,543,000.00 | ||||
NOTE | |||||
DIFFERED PAYMENTS | |||||
ARCHITECTURAL DRAWINGS-MLANDIZI SITE- FOR SCHOOL | 3,500,000.00 | ||||
ARCHITECTURAL DRAWINGS--MAGOMENI- FOR MADRASA | 2,000,000.00 | ||||
BANK A/C NO:00112-00592-20001 | AMANA BANK | ||||
MUNIRA MADRASA &ISLAMIC PROPAGATION ASSOCIATION | |||||
CAPACITY BUILDING | 2013/2014 | ||||
OFFICE MACHINES AND ACCESSORIES | |||||
1 | PHOTOCOPIER MACHINE | 1 | 6,000,000.00 | 6,000,000.00 | |
2 | UPS (STABILIZER) | 1 | 600,000.00 | 600,000.00 | |
3 | SERVICE CHARGES | 400,000.00 | 400,000.00 | ||
4 | PRINTER MULTIPURPOSE | 1 | 980,000.00 | 980,000.00 | |
5 | LAMINATION MACHINE | 1 | 70,000.00 | 70,000.00 | |
6 | BINDING MACHINE | 1 | 75,000.00 | 75,000.00 | |
7 | STAPPLER MACHINE ( H / D ) | 1 | 45,000.00 | 45,000.00 | |
8 | PUNCH MACHINE ( H / D ) | 1 | 25,000.00 | 25,000.00 | |
9 | PAPER CUTTER | 1 | 35,000.00 | 35,000.00 | |
10 | DESK TOP COMPUTERS | 2 | 350,000.00 | 700,000.00 | |
11 | LAP TOP COMPUTER | 1 | 850,000.00 | 850,000.00 | |
12 | DIGITAL CAMERA | 1 | 1,200,000.00 | 1,200,000.00 | |
TOTAL | 10,980,000.00 | ||||
MUNIRA MADRASA &ISLAMIC PROPAGATION ASSOCIATION | |||||
CAPACITY BUILDING | COSTS | MONTHLY | SIX MONTHS | ANNUALLY | |
ADMINISTRATIVE PERSONNEL | |||||
1 | EXECUTIVE SECRETARY | 1 | 300,000.00 | 1,800,000.00 | 3,600,000.00 |
2 | ADMINISTRATIVE SECRETARY | 1 | 200,000.00 | 1,200,000.00 | 2,400,000.00 |
MADRASA TEACHERS | 6 | 900,000.00 | 5,400,000.00 | 10,800,000.00 | |
3 | OFFICE SECRETARY | 1 | 150,000.00 | 900,000.00 | 1,800,000.00 |
4 | OFFICE ASSISTANT | 1 | 100,000.00 | 600,000.00 | 1,200,000.00 |
WATCHMAN | 1 | 180,000.00 | 1,080,000.00 | 2,160,000.00 | |
CAR PARKS REGISTRER | 1 | 150,000.00 | 900,000.00 | 1,800,000.00 | |
TOTAL | 1,980,000.00 | 11,880,000.00 | 23,760,000.00 |
**********************************************************************************
JINA LA TAASISI; MUNIIRA
MADRASA AND ISLAMIC PROPAGATION
ASSOCIATION.
ANUANI; 90536,DAR
ES SALAAM,
SIMU YA MEZANI; 255 222172624
SIMU YA MKONONI; 0713 44 16 39/ 0719
46 47 00/ 0713 43 43 37.
BARUA PEPE; muniiramadrasa@yahoo.com
MTANDAO; www.muniramadrasa.blogspot.com
ACCOUNT;
001120059220001,AMANA
BANK,TANDAMTI BRANCH.
025147013004
– Kenya Commercial Bank, Uhuru Branch,
MAKAZI; MAGOMENI
MAKUTI,
MTAA; KIDUGALO,MAKUTI ‘B’
MANISPAA; KINONDONI,
MKOA; DAR ES
SALAAM.
TAIFA; TANZANIA.
Muniira Madrasa And Islamic Propagation Association ni taasisi ya kidini iliyoanzishwa mwaka
1990 na kupata usajili (No S.A 16751) mwaka 2009 kupitia ofisi ya msajili
wizara ya mambo ya ndani.
Taasisi hii imeanzishwa
kwa sura ya madrasa (ikijulikana kwa jina la Madrasat Muniiral Islamiyyah)
ikiwa na wanafunzi 18 na walimu watatu.
Idadi ya wanafunzi
iliendelea kupanda siku hadi siku kutokana na wazazi na walezi kuridhishwa na
elimu bora,malezi na maadili mema yanayotolewa na madrasa hii.
Taasisi hii
imeanzishwa kwa malengo makuu matatu ambayo ni;-
01-
Kutoa elimu ya kiislamu kwa rika zote.
Katika lengo hili Taasisi hii inatoa elimu
kwa njia mbali mbali ikwemo;-
i.
Kutoa
elimu kwa njia ya darasani (ana kwa ana)
ii.
Kutoa
elimu kwa njia ya vipeperushi,
iii.
Kutoa
elimu kwa njia ya tenzi na mashairi,
iv.
Kutoa
elimu kwa njia ya maigizo ya jukwaani,
v.
Kutoa
elimu kwa njia ya semina,
vi.
Kutoa
elimu kwa njia ya mihadhara,
vii.
Kutoa
elimu kwa njia ya ujumbe mfupi (sms)
viii.
Kutoa
elimu kwa njia ya mtandao (e mail),
ix.
Kutoa
elimu kwa njia ya kutunga vitabu
x.
Kutoa
elimu kwa njia ya ukurasa wa tovuti (blog).
Aidha sasa kwa sasa
Taasisi hii ina endesha Darsa zifuatazo;-
Darsa la
watoto wadogo (wenye umri wa miaka mitatu hadi kumi
Na nane).
Darsa za
wenye umri wa miaka kumi na nane hadi miaka 29.
Darsa la
akina mama kwa umri mchanganyiko.
Darsa la
chekechekea (elimu ya awali).
02-
Kuisaidia jamii inayotuzunguka kwa kadri ya uwezo wetu,
Taasisi hii
inajishughulisha na kuwasidia wana jamii wanaotunguka kwa kuwapatia sehemu ya
mahitaji kwa kadri tunavyomudu.
Fikra hii tumeipata
baada ya kufanya fafiti fupi iliyotupa ufahamu ya kugundua mahitaji waliyo nayo
baadhi ya akina mama hasa wajane na wazee,lakini pia mahitaji yanayowalazimu
watoto yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi.
Katika kuliendea hilo tulichukua hatua ya kuwaorodhesha na hatimaye
kuwafariji kwa hali na mali
kadri ya pale tunapo pata nafasi ya kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa
kumbukumbu za hivi karibuni ni kwamba katika kipindi cha mwaka 2012 na 2013
jumla ya waliosaidiwa na Taasisi hii ni kama
ifuatavyo;-
1.
Wajane
50 walipewa mitaji ya biashara (siyo mikopo) kwa viwango tofauti kati ya
shilingi elfu thelathini na shilingi laki moja kwa kila mmoja.
2.
Wajane wanane
vyarahani vinane.
3.
Wajane
wanne majokofu (frij) manne.
4. Wazee arobaini vyakula (mchele,sukari,sembe
na maharagwe).
5.
Yatima
50,walipewa vyandarua.
6.
Yatima
50 walipewa sare za shule
7.
Yatima 110
walilipiwa ada za masomo (viwango tofauti) katika shule za sekondari.
8.
Watoto
50 walipatiwa matibabu kwa gharama matibabu kati ya shilingi elfu kumi na tano
hadi elfu khamsini.
9.
Kuwatembelea
na kuwafariji wagonjwa mahospitalini (katika siku kuu ya iddil hajj kwa kila
mwaka)
(Tunatoa misaada
hiyo baada ya kuwaomba wapenda kheri na sisi viongozi kujitolea binafsi)
03-
Kusaidiana na serikali katika kufikisha maagizo mema.
Tumekuwa
tunawajibika kusaidiana na serikali katika kufikisha maagizo mema kwa jamii,kama kupiga vita madawa ya kulevya,mmomonyoko wa
maadili,kupinga dhulma,kukemea wizi,ufisadikutoa elimu ya afya nk,
Tumekua tunayafanya
haya kwa kukabiliana na mtu mmoja mmoja au kwa vikundi kwa kutumia njia
mbalimbali ikiwemo ya mihadhara na darsa za ndani.
MAHUSIANO;
Tuna mahusiano
mazuri kati ya taasisi hii na serikali,aidha tuna mahusiano mazuri baina yetu
na Taasisi nyengine zisizo za kiserikali.
MAWASILIANO;
Kwa kufahamu ya
kwamba mawasiliano ni muhimili muhimu katika kufanikisha malengo yetu,mbali ya
mambo mengine tumeweka utaratibu wa kutumia mawasiliano kwa njia zifuatazo;-
- Mawasiliano kwa njia ya barua (sanduku la posta 90536,Dar es salaam)
- Mawasiliano kwa njia ya simu za mkononi
- Mawasiliano kwa njia simu ya mezani
- Mawasiliano kwa njia ya emal
- Mawasiliano kwa njia ya blog
Na
mawasiliano ya ana kwa ana .(tunataraji kuwa na web site ikifika mwaka 2014
inshaa ALLAH)
MALENGO;
Tuna
malengo ya muda mrefu na malengo ya muda mfupi.
Malengo
ya muda mrefu ni pamoja na
1.
Kuwa na
shule yenye hadhi ambayo itakuwa inafundisha kwa wakati mmoja elimu ya dini na
elimu ya mazingira (intergred) kwa ngazi ya awali hadi elimu ya kati,yenye jengo
la utawala,maabara,zahanati,karakana,madrasa,msikiti na nyumba za
maimamu,walimu wa madrasa na walimu wakuu wa shule.
Mwenyeezi
mungu akipenda mradi huu (kwa tathmini ya mwaka 2011,utagharimu Tsh Bilioni
tatu nukta tatu),utakuwa maeneo ya mlandizi wilaya ya kibaha mkoa wa pwani
(tunayo ardhi yenye ukubwa wa heka kumi,taraibu za upimaji na upatikanaji wa
hati umeshaanza).
2.
Kuanzisha
mradi wa kilimo na ufugaji maeneo ya mkuranga,(tulianza mwaka huu kwa majaribio
kilimo cha mihogo,lakini mafanikio hayakuwa mazuri).
3.
Kumiliki
madrasa ya kisasa (eneo la magomeni makuti) yenye vyumba vya madarasa
manne,ofisi mbili,library moja,ukumbi wa mikutano,stoo,vyoo sita na bafu
tatu,(kwa sasa tupo pembezoni mwa nyumba ya msamaria mwema).
MAFANIKIO;
Tangu Taasisi hii
ianzishwe mwaka 1990 hadi kufikia mwaka 2013,kuna mafanikio mengi
yamepatikana,ikiwemo;-
- Kuwaunganisha wazazi wa kiislamu wa maeneo haya na kuwa familia moja.
- Kuwaunganisha watoto wa kiislamu wa maeneo haya na kuwa familia moja.
- Kuwaunganisha wazazi na watoto wa kiislamu wa maeneo haya na watoto na
Wazazi wa kiislamu wa maeneo mengine.
- Kuwafanya watoto na hata wazazi wa kiislamu kuwa na elimu tofauti na hali
Waliyokuwa nayo kielimu na kimaadili kabla
ya kuanzishwa kwa taasisi hii.
- Kuwa na mahusiano mema ya kielimu,kimawasiliano na hata ya kiutendaji na
Na baadhi ya Taasisi mbali mbali na mtu
mmoja mmoja.
- Kuwa na mahusiano mema na serikali.
- Wajane,wazee,wagonjwa,yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu kufaidika na misaada inayotolewa na taasisi.
MENGINEYO;
Taasisi
hii imetenga kila jumamosi ya kwanza katika kumi la mwisho wa mwezi wa Ramadhan,kufuturu
pamoja kama familia moja.
Tukio
hili lina wahusiha waalimu,wazazi,walezi,wanafunzi,wajane,wazee,yatima,watoto
wanaoishi katika mazingira magumu na waislam ambapo takriban watu mia nne
tunafuturu nao pamoja.
usiku
wa kuamkia iddil fit huwa tuna kesha kwa kupita katika majumba ya watu ambao
hali zao ni duni (tumewaorodhesha) na kuwagawia zakaatul fitri kwa lengo la
kuwataka wasinyongeke na wafurahie iddil fitri wao na familia zao.
Ili
kufanikisha zoezi hilo,huwa tunakusanya zakatul fitri kutoka kwa wazazi na watu
wengine.
CHANGAMOTO;
Tunakabiliwa na
changamoto nyingi zikiwemo;-
- Taasisi kutokua na miradi,vyanzo vya mapato.
- Taasisi kutokuwa na uwezo wa kuwalipa waalimu na watendaji wengine (kwani wanajitolea tu).
- Taasisi kutokuwa na jengo (madrasa) la kudumu (hofu yetu inawezekana waliotuhifadhi watakapobadilika kiimani au kimaslahi ikawa ndiyo sababu ya kupotea na kusambaratika kwa mafanikio yote yaliyopatikana katika taasisi hii tokea mwaka 1990 na kuyeyusha ndoto njema kadhaa za taasisi hii,hili linatuathiri sana kifikra).
WITO;
Tunaiomba
serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania,Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,mabalozi
mbalimbali,Taasisi za kiraia,mashirika ya kidini na yasiyo ya kidini ndani na
nje ya nchi,watu binafsi na hata mataifa mbalimbali,kuiunga mkono taasisi hii ili kufikia malengo yaliyojiwekea ambapo tuna
amini malengo haya yakifikiwa itakuwa ni faida kwa jamii mzima ya Watanzania na
Afrika Mashariki.