Feb 16, 2015

BREAKING NEWS;SHULE YA MSINGI JUHUDI INAUNGUA

Kuna taarifa kwamba Shule ya ya Msingi ya Juhudi iliyopo Mbagala Shimo la Mchanga,Manispaa ya Temeke,inaungua.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari moto huo ulianza jana na sasa ndiyo umevamia shule.

"Hapa jirani ya Shule kuna dampo kubwa,sasa tokea jana moto ulikua unawaka katika hili dampo,lakini muda huu ndioyo umeshika shule na ninavyo zungumza madarasa ya kwanza yanaungua na magari ya zimamoto ndiyo yanakuja",kilisema chanzo chetu wakati akiongea na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu;

Habari kamili tutawapatia baadae In shaa Allah

0 comments:

Post a Comment