Dec 10, 2013

Mapigano makali chuo kikuu cha al Azhar

Duru za habari zimearifu kuwa kumetokea mapigano kati ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha al Azhar na askari usalama wa serikali ya Misri na kwamba gari moja limechomwa moto katika mapigano hayo.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha al Azhar ambao ni wafuasi wa Muhammad Morsi, rais wa Misri aliyepinduliwa na jeshi la nchi hiyo, jana waliandamana mbele ya lango kuu la chuo hicho wakilalamimikia kutiwa mbaroni Morsi na vilevile kusekwa jela wanachuo wenzao.


Ripoti zilizotufikia zinaeleza kuwa, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha al Azhar wamelichomota moto gari la Idara Kuu ya Usalama na kuwapiga askari usalama watatu katika maandamano yao ya jana. 

Watu walioshuhudia wamesema kuwa askari usalama wa Misri wametumia gesi nyingi ya kutoa machozi ili kuzima maandamano ya wanachuo hao wafuasi wa Muhammad Morsi. 

Wanafunzi  wa Chuo Kikuu cha Alzhar juzi pia walifanya maandamano  wakilalamikia kutiwa mbaroni Morsi.

 Wanafunzi 100 wa al Azhar wamejeruhiwa na askari usalama katika maandamano ya leo yaliyoibua mapigano makali kati ya pande mbili hizo.

0 comments:

Post a Comment