Dec 23, 2013

MASHEIKH WA DARSA ZA MISIKITINI,BADILISHENI MFUMO-USHAURI




Masheikh wanaoendesha darsa katika misikiti mbalimbali wameshauriwa kubadili mfumo wa ufundishaji.

Ushauri huo umetolewa jana na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Kiislam Morogoro Docta Hamdun Ibrahim.

Amesema masheikh wanaosomesha Darsa Misikitini wamekuwa wakifanya kazi kubwa na mzuri,lakini ni bora waboreshe utendaji wao ili ipatikane natija zaidi.


"Misikiti mingi ina darsa,lakini utakuta miaka nenda miaka rudi vitabu vinavyofundishwa ni vile vile,mimi nashauri tubadilshe mfumo wa ufundishaji ili tukimaliza kitabu hiki tunaanza kitabu kingine na siyo kila mwaka kurudia kitabu hicho hicho"alisema.

Aliongeza kwa kusema "tatizo jengine lipo katika usajili,masheikh wengi hawawasajili wanaosoma katika darsa zao,ifike wakati tuawasajili wanaosoma,na tuwe na taarifa za maendeleo yao,hapa tutaweza kujuwa mambo mengi.

Alimalizia kwa kusema kwa hakika masheikh wetu wanafanya kazi mzuri zaidi,alkini ni vyema wakiongeza uzuri huo kwa kuweka.

Docta Hamdun alikuwa ni mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi vitabu vya kiislamu kwa taasisi zinazo miliki Maktaba,hafla ambayo ilifanyika katika ukumbi wa DYCCC Kariakoo.

0 comments:

Post a Comment