Dec 10, 2013

UAMSHO YALIJIA JUU GAZETI LA AN NUUR



Gazeti la Annuur launga mkono Mauaji yanayofanywa na Bashaar Al Asad nchini Syria.

somalimemo.net 

 Katika hali inayoenesha sintofahamu baina ya taasisi ya UAMSHO yenye makazi yake Zanzibar na Gazeti pendwa la Kiislamu AN NUUR,Munira blog imelazimika kuweka bayana hali hiyo kwa lengo jema ili kila upande uwe tayari kufikia muwafaka katika kuimarisha mahusiano mema ya taasisi zetu,ifuatayo ndiyo hali halisi kama tulivyoinukuu kutoka katika mitandao ya kimataifa.


Nimepitia makala inayoitwa "Ujinga Mzigo" iliyoandikwa na Omar Msangi mhariri wa gazeti ati linaloitwa la Kislamu la Anuur la tarehe 6-12 mwezi huu (uk 3) na kugunduwa
yafuatayo:



1.Anaonesha kuwa Mujahidina ndani ya Syria wanatumika kama walivyotumika baadhi ndani ya Libya, Afghanistan na kwengineko,Kwa hivyo wanaleta balaa, mauwaji na hawana lengo la Uislamu.



2.Mujahidina wananadi kurejesha Khilafah kwa kisingizio cha jihadi ilhali hakuna liwalo.




3.Anaunga mkono hatua ya serikali ya kuwashughulikia na kuwauwa Waislamu wa Kilindi kwa kuwa wana dhana isiyo sahihi ya kutaka kuanzisha khilafah katika vijiji hivyo kwa jihadi kisha kutanua.


Kwanza, ni kweli bwana Omar Msangi tumo katika ujinga mzito kwa sababu zifuatazo:


Tunaendelea kununua gazeti lako lililojivisha guo la Kiislamu kiasi kwamba unalazimika wewe kutoka Arusha, Kirinjiko kwenye shule yako inayoendesha kwa misingi ya ubepari kila wiki kuja Dar tena kwa ndege kuja kuliandaa gazeti hilo kwa kuwa linakuungizia mapesa mengi.



Pili ni kweli tumo katika ujinga mzito uliotukabili kwa kuwa hatukuhoji ulipokwenda Marekani mwaka ule. Ulikwenda kufanya nini na nani alikugharamikia na umepewa majukumu gani baada ya kurudi. Nadhani ilikuwa kwanza utueleze hilo kabla ya kutwambia kwamba makundi ya Kiislamu ndani ya Syria na Libya yanatumika na mkono wa nje.



Sasa angalia Omar Msangi kuchanganyikiwa na kukosa ikhlasi kwako ati Mhariri wa gazeti linaloitwa la Kiislamu


1. Ni kweli kwamba baadhi ya wapiganaji wanatumiwa na mataifa ya magharibi. Hilo halina shaka lakini sio wote. Ukumbuke kwamba upinzani wa Syria umetokana na askari wengi walioasi na kuondoka na silaha na vikosi. Na bado wakaendelea kuteka silaha kila siku.



2. Ni uadilifu wa aina gani unaoufanya Omar Msangi kusema kwamba wapiganaji wanafanya mauwaji makubwa ilhali wao ni wanapigana katika kiwango cha wanamgambo huku serikali inapigana na kila nyenzo za kijeshi na kinguvu?



3. Ni kipimo gani alichotumia Omar Msangi kuonesha kwamba hawa mujahidina wanatumiwa, halafu watawala vibaraka waliotawala kwa ukafiri miaka mingi akiwemo Gadafi na Assad ambae ni mlinzi wa Israel kuwaona kuwa hawatumiwi. Kwa hivyo, aliyetumika miaka mingi zaidi baina ya hawa mujahidina na hawa watawala ni nani?



Jee kuna kutumika zaidi kwa watawala hawa kuliko kutawala kwa ukafiri, kuilinda Israel na kuwauwa walinganiaji Uislamu?



4. Kwa kauli yako Omar Msangi kuwa wapiganaji wanachafua amani na utulivu wa nchi jee mhariri kwa ufahamu wako Kiislamu amani ni nini? Na jee muislamu hupaswa kufanya nini kihukmu anapotawaliwa na twaghut au anapovamiwa na kudhuriwa yeye na familia yake?



5. Ni kweli kuna makundi ndani ya Syria wananadi kutaka kurejesha Khilafah kwa kupitia jihadi . Huko hapana shaka yoyote ni kuchanganyikiwa kwa kuwa jihadi sio njia ya kurejesha dola. Lakini suala la kupigania kurejesha khilafah kwa jihadi. Na kuhubiri ukafiri wa demokrasia ilhali hata hakuna hata malengo ya Uislamu. Lipi ni kuchanganyikiwa kukubwa? Mbona Omar Msangi na gazeti lako la Anuur unaunga mkono mchakato wa kikafiri wa kidemokarasia na wanasiasa wake?.



6. Suala la Kilindi, hakuna muislamu muelewa asiejuwa ikiwa ndugu zetu walikuwa na dhamira ya dola ya Kiiislamu njia waliyopitia wamekosea. Lakini ukweli unabakia wamedhulumiwa. Hata hivyo kukosea kwao
wao na wanaolingania ukafiri wa demokrasia nani kakosea zaidi? Mbona hao wanaolingania ukafiri wa demokrasia unawaunga mkono, kuwasifu na kuwaunga mkono?



7. Msingi ni kuwa Muislamu akidhulumiwa ndugu yako una wajibu wa kumnusuru kisha ndio unamuweka sawa pembeni na sio kumuwacha mkono kama alivyofanya Omar Msangi ati wana malengo ya kusimamisha khilafah kisha kutanua kwa jihadi pia kusema wanatumiwa na serikali.



8. Mwisho tunawaeleza Waislamu waone kwa macho yao namna vinavyojiita vyombo vya habari vya Kiislamu, na huyu Omar Msangi ndio mhariri ambayo hutumiwa na mashia kwa kivuli cha Uislaam bila Umma kufahamu.



Gazeti la Kisiwa walisema mauwaji yaliyofanywa na askari Kilindi Tanga hayakukusudiwa na Anuur nayo wanasema Waislamu wale wanatumiwa na serikali



Tunakwambia Mhariri wa Anuur Bwana Omar Msangi jitahidi zaidi baba upatapata ziara nyengine Marekani. Jitahidi kujitupa mnadani.



Gazeti hili kwa ujumla limedhihirisha wazi kwa yale iliyokuwa ikificha na kujianika hadharani baada ya Uzalendo kumshinda,Wakurungezi wa Gazeti hilo ni Taasisi ya Tampro iliyo na mafungamano na Marekani na Iran na pia Vituo vyao Hupewa Msaada na Marekani na baadhi ya Vifaa vya Vimeandikwa US AID N.K na Huendesha Miradi ya Amref Tanzania.

Imeandaliwa na Vijana wa Jumuia ya Uamsho Zanzibaar kwenye Ukurasa wa Facebook.

0 comments:

Post a Comment