Dec 14, 2013
WAZAZI TUWACHAGULIE WATOTO SAHEMU SAHIHI ZA KUSOMA-USHAURI
Wazazi wa Kiislamu wameshauriwa kuchagua sehemu zenye ubora na maadili kwa ajili ya kuwapatia elimu bora watoto wao.
Hayo yamesemwa na Ustaadh Ally Salum Jongo ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Munira Madrasa And Islamic Propagation Association ya Magomeni Makuti Jijini Dar es salaam.
Akizungumza jana na wazazi katika mahafali ya pili ya wanafunzi wa elimu ya awali (chekechea) alisema,wazazi wasipokuwa na uamuzi sahihi wa wapi sehemu sahihi ya kuwapeleka watoto wao kupata elimu itakuwa ni sawa na kuwatesa watoto hao katika siku za usoni.
"Wazazi wangu,kuna tatizo la kibusara linalo wakabili baadhi ya wazazi kwa kushindwa kuchagua sehemu sahihi za kuwapeleka watoto wao kupata elimu,hii itawatesa watoto wetu siku zijazo",alisema.
"Ukiwa ni mzazi unapaswa ujuwe unampeleka mtoto wako shule gani kwa sasa,na akitoka hapo anakwenda katika shule ya aina gani inayo lingana na alipotoka"alisema
Aliendelea kufafanua,"ninao ushahidi wa wazi,kuna watoto walisomeshwa katika shule za awali zinazo tumia mchepuo wa kiingreza,lakini watoto hao walipopelekwa shule za msingi zisizo tumia mchepuo wa kiingreza,matokeo yake walipata tabu sana na wakaanza upya,kwani walichofundishwa sicho walicho kikuta".alisema.
Alikwenda mbali zaidi kwa kusema pia "zipo shule ambazo zina wahifadhisha watoto lugha na namba lakini haziwafundishi kujuwa lugha na namba hizo,sasa hili ni tatizo la kiutaalamu"
"Nawapongeza sana wazazi mulioamua kuwaleta watoto wenu katika kituo hiki,kwani watoto hawa wanajuwa kusoma na kuandika,Japo baadhi yao wamekataliwa kujiunga shule za msingi kwa kuwa umri wao ni mdogo lakini wana juwa kusoma na kuandika vizuri"mwisho wa kumnukuu.
Munira Day Care And Nursery School ni kituo chenye maadili ya Kiislamu na kina fundisha kwa mchepuo wa kiingreza,kiswahili na kiarabu.
Aidha katika kujipanga zaidi hapo mwakani (In Shaa ALLAH),kituo hicho kina kusudia kuongeza madawati,mabembea na magodoro kwa ajili ya kuwapatia huduma bora watoto wa Kiislamu.
USTAADH ALLY SALUM JONGO MWENYEKITI WA TAASISI YA MUNIRA MADRASA AMBAYE ALIKUWA MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI HAYO,AKIMKABIDHI RIPOTI MMOJA WA WAKHITIMU HAO.
MWALIMU ZAINAB (AMBAYE NI MWALIMU MKUU) AKIMKABIDHI ZAWADI MMOJA WA WAKHITIMU.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment