Sep 3, 2014

Saudia kubomoa kaburi la Mtume Muhammad (s.a.w)

Gazeti la Independent la nchini Uingereza limefichua mpango unaoandaliwa na Saudi Arabia wa kubomoa kaburi la Mtume Muhammad (s.a.w) lililoko Masjid al-Nabawi mjini Madina.
Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na gazeti hilo ni kwamba, msomi mmoja wa Saudi Arabia ametoa pendekezo la kubomolewa kaburi la mtume na mabaki yake kuzikwa upya kwa siri katika makaburi ya al-Baqi. 

Ripoti hiyo pia inafichua kwamba, msomi huyo wa Saudia amependekeza kuharibiwa vyumba vilivyokuwa vikitumiwa na watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w) yaani Ahlul Bayt (a.s) sambamba na kuvunjwa Kuba ya Kijani ambayo ndiyo nembo ya msikiti wa Mtume (s.a.w). 

Kwa sasa duru za karibu na ufalme wa Saudia zinaarifu kuwa, pendekezo la msomi huyo linajadiliwa na kwamba kuna uwezekano mkubwa likawasilishwa kwa Mfalme Abdullah kwa ajili ya maamuzi ya mwisho

Mpango huo unatarajiwa kuamsha hasira za Waislamu kote duniani kwani waumini wengi huenda mara kwa mara kufanya ziara kwenye kaburi la Mtume Mtukufu pamoja na kufanya ibada katika Masjid al-Nabawi; eneo ambalo ni la pili kwa utukufu baada ya Masjid al-Haram mjini Makka.

0 comments:

Post a Comment