Katika ripoti yake Amnesty International imesema kuwa, makumi ya watoto wamekumbwa na vitendo vya kuteswa na kupigwa vikali na utawala wa kifalme wa nchi hiyo tangu mwaka 2011.
Naibu Mkuu wa shirika hilo katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika Said Mamdouh ameutuhumu utawala huo wa Bahrain kwa vitendo hivyo vya kuwatesa watoto na kutaka utawala huo uwajibishwe katika taasisi za kimataifa za kutetea haki za binaadamu.
Ameitaka serikali ya Manama kuwaachilia huru watoto wote walio chini ya umri wa miaka 18 sanjari na kuitaka serikali hiyo ya kidikteta kufanya uchunguzi kuhusiana na vitendo hivyo.
Watoto wasiopungua 110 walio na umri kati ya miaka 16 na 18 wanashikiliwa katika jela za utawala wa Aal-Khalifa.
0 comments:
Post a Comment