- SINA TAARIFA KAMA POLISI WANA NITAFUTA.
- SI DAWA YA KUNIZUWIA KUTETEA HAKI ZA WAISLAMU.
Na mwandishi wetu wa munira.
Katibu mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda amesema Polisi ndiyo walionipiga risasi.
Sheikh Ponda ameyasema hayo jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipofikishwa kwa ajili ya matibabu,"Polisi wamenipiga risasi lengo lao ni kuniuwa,lakini kwa uwezo wa ALLAH nimenusurika".
Alieleza ya kwamba hakukuwa na sababu ya msingi ya kunipiga risasi kama kweli wana nitafuta wana juwa napatikana wapi,lakini sina taarifa zozote za kutafutwa wala barua ya mimi kuitwa polisi,nayaona haya katika vyombo vya habari tu,alisema.
"Pamoja na hili lililotokea napenda ifahamike hii si dawa ya kunizuwia kupigania haki",alisema.
Kwa upande wake Jeshi la Polisi kupitia kwa kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile alikanusha madai hayo jana Asubuhi alipoongea na mwandishi wetu kwa njia ya simu.
Katika hatua ya kushangaza polisi walionekana kutanda katika Hospitali hiyo tokea asubuhi kwa madai ya kutaka kumkamata,hadi mwandishi wa munirablog anaondoka eneo la tukio sheikh ponda alikuwa katika chumba cha upasuaji MOI.