Aug 7, 2014

UGANDA KURUDISHA USHOGA?


Wabunge wa Uganda wanafanya jitihada za kupasisha tena sheria inayopiga marufuku vitendo vya ushoga na maingiliano ya ngono kati ya watu wenye jinsia moja.

Mbunge Abdu Latif Ssebaggala wa Uganda ameviambia vyombo vya habari kwamba zinafanyika juhudi za kupata saini zinazohitajika za kupasisha tena sheria inayopiga vita ushoga katika bunge hilo. 

Ssebaggala amesema anatarajia kupata saini za wabunge 200 kati ya 383 zinazohitajika kwa ajili ya kupasisha tena sheria hiyo ambayo ilibatilishwa na Mahakama ya Katiba wiki iliyopita baada ya kubainika kuwa ilipasishwa bila ya kuhudhuria idadi inayotakikana ya wabunge. 

Sheria hiyo ilipasisha adhabu ya kifungo cha maisha kwa watu wanaojamiiana wakiwa na jinsia moja.

Nchi nyingi za Afrika zinapiga marufuku maingiliano ya ngono baina ya watu wenye jinsia moja.

0 comments:

Post a Comment