Dec 16, 2013

TUTAWASAIDIA AL HARAMAIN-MUNADHWAMAT DAAWAT





 MKUU WA KITENGO CHA DINI KATIKA SHULE YA AL HARAMAIN SHEIKH TWAHA BANE AKIPOKEA ZAWADI MAALUM KUTOKA KWA MGENI RASMI DOCTOR KHALID

Ahadi ya kukisaidia kitengo cha dini cha ALharain Islamic centre imetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akiongea katika mahafali ya wakhitimu wa Thanawy (kidato cha sita) shuleni hapo,mkurugenzi wa taasisi ya Munadhamat Daawat yenye makao makuu nchini Sudan Doctor Khalid Al Awadh amesema taasisi yake ipo tayari kuisaidia Al Haramain.


"Licha ya kuwapongeza wakhitimu hawa,lakini tunaahidi kutatua sehemu ya changamoto zinazo kikabili kitengo cha dini",alisema.

Aliendelea kusema kwamba "kwa kuanzia tutatoa Computer tano mwanzoni mwa mwaka 2014,tutawapatia semina,tutawapatia vitabu na wanafunzi wote waliofanya vizuri tupo tayari kuwapeleka na kuwasomesha nchini Sudan kwa gharama zetu".alisema.

Aliwahakikishia wahitimu wote waliokidhi vigezo watawasaidia kupata nafasi katika vyuo vikuu vya ndani ikiwemo chuo cha Chwakwani Zanzibar,Dodoma na Morogoro.

Wakati huo huo mkurugenzi huyo amekipongeza kitengo cha dini cha Al haramain kwa kazi nzuri wanayoifanya.

"Kwa sasa mtu hawezi akasema kwamba hajui elimu ya dini,sisi Munadhamat kwa kushirikiana na kitengo cha dini cha Al haramain,tumeweza kutafsiri vitabu vya dini kwa lugha ya Kiswahili".

"Kwa hili nampongeza sheikh Doga,shekh Bane na wenzao kwa kazi nzuri ya kutafsiri kwa lugha ya kiswahili vitabu zaidi ya ishirini"mwisho wa kumnukuu.
















0 comments:

Post a Comment