Jul 1, 2014

Misri: mashambulizi karibu na ikulu ya Cairo yaua maafisa wa polisi

Abdel Fattah al-Sissi, rais wa Misri.
Abdel Fattah al-Sissi, rais wa Misri.

Mabomu zaidi ya mawili yamelipuka karibu na ikulu ya rais mjini Cairo na kuua maafisa wawili wa polisi na kujeruhi watu wengi, chanzo cha usalama kimearifu.

Kundi la wanamgambo wa kislamu Ajnad Masr lilikiri hivi karibuni kutekeleza mashambulizi yaliyoutikisa mji wa Cairo na kutahadhari kuwa lillitega mabobu karibu na ikulu ya rais, ilioko mashariki mwa mji wa Cairo, huku likithibitisha kwamba halitayalipua kwa kuhofia usalama wa raia.

Mapema asubuhi afisa wa polisi ameuawa katika mlipuko wa bomu uliyotokea karibu na ikulu, imethibitisha chanzo cha usalama.

Saa moja baadae, askari polisi walijaribu kutegua bomu liliyokua limetegwa bila hata hivo kufaulu, kwani lililipuka kabla zoezi lao halijakamilika, na kusababisha kifo cha afisa mwengine wa polisi na kuwajeruhi askari polisi wengi, huku mtu mmoja ambae amekua katika shughuli za uokozi akijikuta mkono wake umedondokea chini.

Juma liliopita, milipuko mitano ilitokea katika vituo vya treni na kusababisha vifo vya watu wawili na wengine sita kujeruhiwa. Mahakama moja ya Cairo na kituo cha mawasiliano ndivyo vilikua vililengwa na mabomu hayo.

Mashambulizi ya jumatatu hii yanatokea wakati mwaka moja unakamilika tangu zaidi ya raia wa Misri milioni moja kuandamana wakimtaka rais Muhamed Morsi kutoka chama cha Muslim Brootherhood ajiuzulu.

Maandamano ya kumpinga rais Mohamed Morsi.
Chama hicho cha udugu wa kislam kilitangazwa hivi karibuni na utawala wa Abdel fatah al Sissi kuwa ni kundi la kigaidi. 

Muhamed Morsi anatuhumiwa kujaribu kujipa madaraka mengi kwa faida ya kundi hilo la Muslim Brothershood na kuweka sheria za kislam nchini Misri.

Lakini siku tatu baadae, Julai 3, Muhamed Morsi aling'olewa madarakani na kukamatwa kwa amri ya aliekua kiongozi wa jeshi Abdel Fatah Al Sisi, ambae alichaguliwa rais wa Misri mwezi Mei.

Wafuasi wa rais Mohamed Morsi wakikabiliana na polisi mjini Cairo mwaka 2013.
Tangu Muhamed Morsi atimuliwe madarakani, askari polisi na wanajeshi waliwaua wafuasi wake 1,400 ambao walikua wakidai arejeshwe madarakani, huku zaidi ya wafuasi 15,000 wakiziwiliwa jela na mamia wakihukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha jela.

0 comments:

Post a Comment