Wakati mwezi mtukufu wa Ramadhan ukiwa umeanza, Kamishna Mkuu wa
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Antonio Guterres, ametuma salamu
zake kwa Waislamu wote na kuwatakia mfungo mwema, huku akisema kuwa
mwaka huu mwezi wa Ramadhan umekuja wakati ulimwengu unaposhuhudia
ongezeko la watu waliolazimika kuhama makwao kwa viwango ambavyo
havijashuhudiwa katika miongo mingi.
Bwana Guterres amesema kutoka Mali, Sudan Kusini, Syria hadi
Afghanistan, watu zaidi ya milioni 50 sasa wamelazimika kuhama makwao,
wengi wao wakiwa wanatoka au wanapewa hifadhi katika nchi za Kiislamu,
"Na nyingi ya nchi hizo zimeonyesha ukarimu mkubwa, katika moyo
wa mshikamano na ulinzi wa wanyonge, ambao unatokana na utamaduni wa
uislamu, kama ilivyoandikwa katika Koran takatifu na mafundisho ya Mtume
Mohamed, Amani iwe naye.
Na nina imani kuwa usaidizi huu utaendelea.
Nawatakia tena na familia zenu mwezi mtukufu wa Baraka. Ramadhan
karimu."
Jul 1, 2014
Guterres kwa Waislamu: Ramadhan Karimu na endeleeni kuwasaidia Wakimbizi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment