kufuatia Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe John Magufuli kuteua na kutangaza wakuu wa Mikoa,uteuzi huo umepokewa kwa hisia tofauti.
Uchunguzi uliofanywa jana na Munira blig umebaini kwamba baadhi ya wananchi wanasifia uteuzi huo huku wengine wakiukosoa.
Akiongea na Munira blog,Ndugu Mikadai Issa Mkazi wa Ilala Mchikichini alisema, uteuzi huo ni mzuri na umezingatia kasi ya Serikali ya awamu ya tano.
Alitoa mfano kwa mkuu wa Mkoa wa Kinondoni Mhe Paul Makonda ni kijana mchapakazi anaye endana na kasi ya awamu ya tano.
Kwa upande wake Ndugu Mosha Andrea mkazi wa Kimara alisema uteuzi huo umegubikwa na Siasa za ha Hali ya juu huku akishutushwa naUtamaduni wa Wanajeshi kupewa dhamana ya kuongoza baadhi ya mikoa akidai ni kuwadhibiti Wapinzani.
"Sijafurahishwa na sehemu kubwa ya uteuzi huu,kwani natafsiri ni utauzi uliojaa siasa ambapo sitegemei mabadiliko zaidi ya kuimarisha chama chao na kukandamiza upinzani",alisema Ndugu Mosha.
Naye Bwana Majid Suleyman mkazi wa Temeke amesema uteuzi huu unazidi kumpa mashaka kutokana na kutanuka kwa pengo kubwa la uwiano wa kidini.
Akifafanua Ndugu Majid alisema,"katika wakuu wa mikoa 27 majina ya waislamu hayazidi matano au sita,sitaki kuamini kwamba hatuna sifa ya kushika nyadhifa hizo".
Aliendelea kusema kwamba hata Uteuzi wa Wakuu mbalilmbali kuanzia Baraza la Mawaziri,manaibu,makatibu wakuu nk,namba ya waislamu imekua ndogo sana ukilinganisha na uhalisia,hii inanipa mashaka makubwa na awamu huu.mwisho wa kumnukuu.
Mar 15, 2016
UTEUZI WA WAKUU WA MIKOA WAPOKEWA KWA HISIA TOFAUTI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment