Aug 7, 2014

Sheikh Abuu Ismail Ibrahim,Imam wa Masjid Quba na Waislaam Kadhaa wafikishwa Mahakamani Arusha.

MmojawaWaislaamwaliofikishwaMahakamaniakionyeshaKidole chaKalimayaTawheed.
 
Kwa mara ya kwanza tangu alipovamiwa na kutekwa na Maaskari wa kupambana Uislaam tarehe 13,July,2014, uisku wa manene katika Nyumba na Markazi ya kufundishia Madrasa uliopo jijini Mwanza Sheikh Maarufu miongoni mwa Madaia wa Haqi Sheikh Abuu Ismail Ibrahim na baadhi ya Waislaam hivi karibuni wamefikishwa kwenye Mahakama mjini Arusha.
Shekhe na baadhi ya Waislaam akiwemo mwanadada Sumaya na mumeo wanakabiliwa na tuhuma ambazo hakuna ushaidi na Mahakama imeakhirisha hadi 15 August mwaka huu itakapotajwa tena.

Katika siku za hivi karibuni Serikali kibaraka ya Tanzania imekuwa ikiwasakama Waislaam waishio Nchini kwa kuwahusisha na milipuko mbalimbali yalioitikisha katika baadhi ya miji mikubwa hapa nchini.

Upande wa Sheikh Abuu Ismail anatuhumiwa katika kesi aliyomwagiwa tindikali Mustapha Kihago na ulipuaji wa mwisho wa Hoteli mmoja iliyopo jijini Arusha la Night Park pamoja na kile walichokitaja kueneza Mawaidha yalio na uchochezi kwenye mtandaoni.

Hata hivyo Imam wa Mskiti wa Quba Sheikh Ja'far Lema nae amefikishwa Mahakama akituhumiwa kesi kama ya Shekhe Abuu Ismail Fakallahu Asra.

Wadadisi wa masuala ya usalama wanasema Serikali ya Tanzania namna inavyoshugulikia Kesi na kuwakamata watu wasio husika kwenye kesi hizo ni kuendelea kuchochea zaidi na ulipuaji wa maeneo zaidi yatakayolengwa upya katika nchi hiyo iliyopo Bara la Afrika Mashariki.
 
Habari hizi kwa msaada wa mtandao wa somali

0 comments:

Post a Comment