Msikiti wa Mtambani uliopo maeneo ya kinondoni jijini Dar es salaam umeteketea kwa moto.
Tukio hilo la kusikitisha na kuhuzunisha limetokea jioni hii muda mfupi mara baada ya swala ya na kuzua taharuki kubwa.
Munira blog ilifika na kushuhudia moto mkubwa ukiwaka ambao tayari ulikua umeteketeza ghorofa ya kwanza ambayo hutumika kwa matumizi ya shule.
Kwa mujibu wa mashuhuda walioshuhudia tukio hilo tokea mwanzo wamemwambia mwamdishi wa habari hizi kwamba moto huo umeanzia juu kwa maana shuleni.
"Mara baada ya kuswali tukaanza kusikia kelele kutazama moto unawaka juu na haraka tukakimbilia kuwatoa baadhi ya wanafunzi wachache waliobakia kwa masomo ya ziada",alisema kijana mmoja ambaye hakuweza kutaja jina lake.
Kwa mujibu wa taarifa zaidi ni kwamba gari ya zima moto zilifika mbili lakini ziliishiwa maji na kuondoka.
Munira blog ilimpigia simu kamanda wa polisi kanda maalumu Suleyman Kova lakini simu yake iliita bila ya majibu.
Aidha hali ilikuwa hivyo hivyo kwa mseamji wa jeshi la polisi.
Baadhi ya waislamu wamevitupia lawama vyombo vya ukoaji kwa kutokuonyesha ushirikano wa kutosha.
"Hii ni hujuma,leo kuna vyombo vingi vya uwokoaji lakini wamekuja fire peke yao,viko wapi vyombo binafsi",alisikika bwana mmoja akilalama.
Munira blog ilishuhudia akina mama na baadhi ya wanao hisiwa kuwa ni wanafunzi wakilia kwa uchungu na kulazimika kupata msaada wa kubebwa na kubembelezwa kutoka kwa wasamaria wema.
kwa upande mwingine jeshi la polisi liliimarisha ulinzi eneo zima linalozunguka msikiti huo.
Wakati huo huo Sheikh Omar Al had ambaye kwa sasa yupo eneo la tukio anaripoti ya kwamba waislamu wamechukua hatua ya kuuzima moto kwa kutumia ndoo za maji.
kwa mujibu wa taarifa aliyonitumia hivi punde anasema kuna misururu mirefu ya waislamu wakiwa wamebeba ndoo za maji na kuyaingiza katika gari la zimamoto huku wangine wakijitosa kwenda kuzima wenye.
"kwa hakika inatia faraja kuona waislamu wamehasika na kupanga foleni ndefu kumimina maji katika gari ya zima moto na wana fanya hivyo kwa kasi kubwa sana,nathubutu kusema kwa njia hii moto umedhibitiwa".almekhitimisha sheikh Omar Al had.
PICHA ZITAWAJIA HIVI PUNDE IN SHAA ALLAH
Aug 13, 2014
INNAA LILLAAH WAINNAA ILAYHI RAJIUUN; MSIKITI WA MTAMBANI UMETEKETEA KWA MOTO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment