Jun 30, 2014

Waislamu waanza kufunga Ramadhan

Waaumini wakati wa kufturu mwezi wa Ramadhan nchini Sudan. Waaumini wakati wa kufturu mwezi wa Ramadhan nchini Sudan.

 Waislamu wanaokadiriwa kufikia bilioni 1.6 duniani jana Jumapili (29.06.2014) wameanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ambapo hujizuwiya kula na kunywa kwa kutwa nzima na kuepuka kila aina ya maovu

Mwezi huu mtukufu umegubikwa na machafuko ambayo hayakuwahi kushuhudiwa kabla ya umwagaji damu na uhasama wa madhehebu wenye kutishia kuisambaratisha Mashariki ya Kati ambacho ni kitovu cha Uislamu.

Damu inamwagika nchini Syria. Wanamgambo wa itikadi kali wameteka sehemu kubwa ya ardhi ya Iraq.Lebanon,Libya, Pakistan,Afghanistan na Misri zote zinapambana na Waislamu wa itikadi kali.

Mamilioni ya wakimbizi wa vita hivyo wametawanyika kila mahala.
Juu ya kwamba umwagaji damu umeiondosha kwa kiasi kikubwa raha ya Ramadhan,mamilioni ya Waislamu watafunga kwa masaa kwa kutaraji msamaha wa Mwenyenzimungu.

Ramadhan ni nini ?
Ni mwezi wa mtukufu wa kufunga ambapo kwayo Waislamu wanajinyima chakula, maji ya kunywa na aina nyengine ya starehe kuanzia jua linapokuchwa hadi macheo. 

Ramadhan ni mwezi ambao Waislamu wanaamini kwamba Mwenyeenzimunga alianza kumteremshia Quran Mtume Muhammad (SAW).

Kwa waumini huu ni mwezi wa tafakuri na ibada,kukumbuka shida za wengine na kutowa sadaka.

Kuanza na kumalizika kwa Ramadhan
Waumini wakati wa sala mwezi wa Ramadhan Cameroon. Waumini wakati wa sala mwezi wa Ramadhan Cameroon.

Uislamu unafuata tarehe ya muandamo wa mwezi kwa hiyo kuanza kwa Ramadhan kunatafautiana kila mwaka. 

Mwezi huu huanza kuadhimishwa mara tu baada ya kuonekana kwa mwezi mchanga. 

Kuonekana kwa mwezi mpya mwishoni mwa mwezi wa Ramadhan kunaashiria siku kuu ya Idd al- Fitr tamasha la siku tatu la kuadhimisha kumalizika kwa Ramadhan.

Kwa nini Waislamu wanafunga?
Funga ni mojawapo ya nguzo tano za Uislamu.

Waislamu wanataja sababu nyengine za kufunga ni pamoja na : kujifunza hisia za maskini,kujifunza namna ya kuidhibiti nafsi na kujisabilia kwa Mwenyeenzimungu.

Uislamu hauruhusu wazee, watoto, wanawake wajawazito,wagonjwa au wasafiri kufunga.

Katika baadhi ya nchi kama vile Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu watu wasio Waislamu hawaruhusiwi kula,kunywa au kuvuta sigara hadharani wakati wa mwezi wa Ramadhan.

Nchi nyengine msimamo huo umeregezwa.

Muumini akisoma Quran mwezi wa Ramadhan nchini Yemen. Muumini akisoma Quran mwezi wa Ramadhan nchini Yemen.
Ramadhan na vurugu
Wanamgambo wa Kisunni nchini Iraq huko nyuma wamekuwa wakiongeza mashambulizi yao wakati wa mwezi wa Ramadhan kwa imani kwamba mashambulizi hayo hususan ya kujitowa muhanga wakati wa Ramadhan huwa yana baraka kubwa na thawabu kubwa zaidi kutoka kwa Mungu.
Ibada katika mwezi wa Ramadhan mjini Mecca Saudi Arabia. Ibada katika mwezi wa Ramadhan mjini Mecca Saudi Arabia.

Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia jana Jumapili amewashutumu watu wenye itikadi kali za kidini na kuahidi kutowaachilia magaidi wachache wawatishe Waislamu.

Katika hotuba yake ya kuukaribisha mwezi wa Ramadhan amesema Uislamu ni "dini ya umoja,udugu na kusaidiana" lakini baadhi ya watu wakidanganywa na wito usio sahihi wanaelewa vibaya mageuzi kwa kuyachanganya na ugaidi.

Amesema lengo lao ni kutia chokochoko miongoni mwa Waislamu akimaanisha kundi la wanamgambo la Dola la Kiislamu la Iraq na Sham (ISIS).

0 comments:

Post a Comment