Majambazi wawili kati ya watatu wakiwa na silaha aina ya bastola wamekatwa.
Tukio hilo limetokea mchana huu maeneo magomeni makuti manispaa ya kinondoni mkoa wa Dar es salaam.
Kwa mujibu wa mwandishi wetu munira Blog Fahme Ferej ambaye alishuhudia tukio hilo anasema,polisi walipata taarifa juu ya kuwepo kwa majambazi hao na baada ya kuwafuatilia walianza kukumbia.
Lakini kutokana na ushirikiano mwema kutoka kwa raia wema majambazi hayo yalitiwa nguvuni.
Katika hali ya kujiokoa na kupoteza ushahidi,mmoja wa majambazi hayo alikmbilia katika nyumba moja na kuitupa Bastola chooni,lakini wananchi walikuwa imara na kumkata.
Mwandishi wetu alishuhudia mmoja kati ya majambazi watatu akikimbia kuelekea kusikojulikana huku wengine wakifikishwa katika kituo cha Polisi magomeni.
Munira Blog ilimpigia simu Hamis Kullata ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa makuti "B" ili kuthibitisha tukio hilo ambapo alisema hakuwepo ila amesikia taarifa kutoka kwa wananchi.
Munira blog ilipompigia kamanda wa polisi kanda maalum Suleyman Kova Ili kuthibitisha tukio hilo,aliomba apigiwe baadae.
Hapo ni baada ya Jambazi kukimbilia ndani ya Nyumba kujificha na Silaha kuitumbukiza ndani ya shimo la Choo.
Huyu ni Jambazi wa pili [2] aliyekamatwa na Wananchi.
Hapo ni baada ya wanausalama kukamilisha kazi na kuwapeleka Majambazi hao katika Kituo kikubwa cha Polisi Magomeni.
HABARI NA PICHA KUTOKA KWA MWANAHABARI WETU-SAID MOHAMMED Na FAHME FEREJ
0 comments:
Post a Comment