Jul 1, 2014

Kasisi mashuhuri Australia ajiuzulu kwa kubaka


Kasisi mwandamizi wa kanisa Katoliki nchini Australia, Max Davis, amejiuzulu baada ya kufikishwa kortini kujibu tuhuma za kuwalawiti watoto wadogo. Imedaiwa kuwa, Max Davis alimlawiti mwanafunzi aliyekuwa na umri wa miaka 13 katika chuo cha Saint Benedict mwaka 1969.
Kasisi huyo amekanusha tuhuma hizo na kusisitiza kuwa hajawahi kuhusika na uozo huo.

Kashfa za makasisi wa Kikatoliki kuwadhalilisha kingono watoto wadogo imezusha mpasuko mkubwa kwenye kanisa hilo huku baadhi ya ripoti zikionyesha kuwa, makao makuu ya kanisa hilo (Vatican) imekuwa ikificha makusudi uozo huo ili kulinda heshima yake. 

Mwaka uliopita, Kadinali mwandamizi wa Australia alikiri kwamba, ofisi yake imekuwa ikiwakingia kifua makasisi waovu kwa hofu ya kusambaratika kanisa hilo.

0 comments:

Post a Comment