Idadi ya watu waliouawa katika wimbi jipya la machafuko katika
Jamhuri ya Afrika ya Kati imeongezeka na kufikia watu 70.
Maafisa wa Mpango wa Kimataifa na nchi za Afrika wa kusaidia Jamhuri ya Afrika ya Kati (MISCA) wamesema kuwa, watu karibu 70 wameuawa wiki hii katika eneo la Bambari na vijiji vya pambizoni, huku wengine wasiopungua 100 wakijeruhiwa na nyumba karibu 150 kuchomwa moto.
Machafuko hayo yalianza baada ya magaidi wa Kikiristo wa Anti- Balaka kuua Waislamu 17 wa jamii ya Fulani karibu na mji huo.
Katika upande mwingine Jumuiya ya Kimataifa ya Haki za Binadamu imeripoti kwamba, wanaofanya ukatili na jinai dhidi ya binadamu wanasamehewa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Jumuiya hiyo aidha imesema, magaidi wa Anti Balaka wanaratibu mashambulizi dhidi ya Waislamu nchini humo.
Hayo yanajiri huku nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Katikati mwa Afrika (ECCAS) zikipanga kujadili mgogoro wa Jamhuri ya Kati katika mkutano wao utakaofanyika nchini Equatorial Guinea.

0 comments:
Post a Comment