Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Yussuf Ilembo
JESHI la Polisi Zanzibar, linawashikilia watu saba kwa tuhuma za
kutekeleza shambulizi la bomu katika maeneo ya Darajani na kusababisha
kifo cha mtu mmoja na wengine saba kujeruhiwa.
Akizungumza na gazaeti hili ofisini kwake Ziwani, Naibu Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa jeshi la polisi, DCI, Yussuf Ilembo
,alisema watuhumiwa hao walikamatwa Juni 18 mwaka huu majira ya usiku
katika maeneo mbali mbali ya mi wa Zanzibar.
Hata hivyo, alikataa kutaja majina ya watuhumiwa hao akisema bado upelelezi unaendelea.
Alisema watuhumiwa wamepelekwa makao mkuu ya polisi Dar es Salaam kwa mahojiano.
Aliwataka wananchi kuacha kufuata vishwawishi na kurubuniwa na watu
au makundi ya kihalifu kwa lengo la kuchafua amani na kuwatia hofu
wananchi.
Tukio hilo la bomu lilitokea wika Juni 13 majira ya saa 2:30 za usiku
katika maeneo ya Darajani ya mjini Unguja na kuwalenga wahubiri wa
amani wa dini ya kiislamu waliokuwa nje ya msikiti.
Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Kassim Issa Muhammed (36) ,Hamad
Nassor Kassim (46) , Khelef Abdalla Abdalla (21), Khalid Ahmed Haidar
(16) , Ahmed Haidar Jabir (47) na Suleiman Ali Juma (21) huku marehemu
akitambulika kwa jina la Mohammed Khatib Mkombalaguha (26) mwenyeji wa
Tanga.
Jun 28, 2014
7 mbaroni wakituhumiwa kuripua bomu Darajani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment