Jun 29, 2014

'Marekani inachochea machafuko nchini Iraq'


Magaidi wa Daesh Magaidi wa Daesh
Kamanda mwandamizi wa kijeshi nchini Iran amesema machafuko yanayoendelea hivi sasa nchini Iraq ni mfano wa 'vita vya niaba' vya Marekani Mashariki ya Kati huku akisisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakabiliana kwa nguvu na tishio lolote dhidi ya nchi hii.
Akizungumza Jumamosi, Brigedia Jenerali Masoud Jazayeri Naibu Mkuu wa Vikosi vya Kijeshi Iran amesema vita vya niaba au vita wakala katika Mashariki ya Kati vinaongozwa na watawala wa Marekani wakishirikiana na baadhi ya nchi za eneo kama vile Saudi Arabia. 

Kamanda huyo mwanadamizi nchini Iran amesema Marekani inaeneza ugaidi duniani kwa malengo yake haramu ikiwa ni pamoja na kuuhami utawala haramu wa Israel.  

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Ryabkov amezionya nchi za Ulaya na Marekani kwamba makundi ya kigaidi sasa ni hatari kubwa kwa usalama wa Mashariki ya Kati. 

Amesema Russia haitakaa na kuangalia tu makundi ya kigaidi yakivuruga usalama katika eneo. 

Hayo yanajiri wakati ambao serikali ya Iraq imetangaza kupokea ndege za kisasa za kivita zilizotengenezwa Russia aina ya Sukhoi kwa lengo la kukabiliana na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu la Iraq na Sham kwa kifupi Daesh. 

Serikali ya Iraq imeokosoa Marekani kwa kuchelewa kutuma ndege aina ya F-16 ambazo ilikuwa imeagiza na kusema kuchelewa kufika ndege hizo kumechangia magaidi wa Daesh kuuteka mji wa Mosul. 

Jana Jeshi la Iraq liliitangaza kufanikiwa kuchukua udhibti wa mji wa Tikrit uliokuwa mikononi mwa magaidi wa Daesh.

0 comments:

Post a Comment