Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa
Mataifa ameeleza kuwa malundo kwa malundo ya viwiliwili vimetelekezwa
baada ya kujiri mauaji ya umati huko Sudan Kusini wiki iliyopita.
Toby
Lanzer Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na misaada
ya kibinadamu amesema kuwa viwiliwili vingi vya wahanga wa mauaji hayo
viko misikitini na hospitalini na kutelekezwa huko katika mji wa Bentiu,
makao makuu ya mkoa wa Unity unaozalisha mafuta nchini Sudan Kusini,
baada ya kabila la Nuers kufanya mauaji ya umati tarehe 15 na 16 mwezi
huu.
Lanzer amesema hii ni mara ya kwanza
kuwa na taarifa kwamba, kituo cha redio cha kieneo kilikuwa kikitangaza
ujumbe wa chuki unaowahimiza watu kushiriki katika uovu huo.
Ameongeza
kuwa maelfu ya wakimbizi kutoka makundi tafauti ya kikabila wanakimbilia
kwenye makao makuu ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa
huko Bentiu kwa ajili ya hifadhi, huku wengine wengi wakiamini kuwa
machafuko zaidi yanakuja.
Kituo hicho cha walinda amani wa Umoja wa
Mataifa kinawahifadhi watu 22, 000.
0 comments:
Post a Comment