Wanajeshi wa Uganda wamemtia nguvuni
afisa wa Kundi la Wanamgambo wa Kikristo wa LRA na kuwakomboa mateka
kumi.
Msemaji wa jeshi la Uganda Paddy Ankunda ameeleza kuwa afisa huyo
wa LRA kwa jina la Charles Okello amepelekwa rumande huko kusini
mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Ankunda amemtaja Okello
kuwa ni kamanda wa kivita wa kundi la Kikristo lenye sifa mbaya la LRA
na kuongeza kuwa kilicho muhimu ni kuwa, wamewakomboa watu kumi, ambao
ni watoto saba na wanawake watatu, waliokuwa wakishikiliwa mateka na LRA
kwa muda wa miezi sita.
Itafahamika kuwa, jeshi la Uganda
limekuwa likiongoza kikosi cha Umoja wa Afrika kilichopewa jukumu la
kuwasaka na kuwatia nguvuni wanachama wa LRA, huku baadhi yao wakisakwa
kwa udi na uvumba na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ya mjini the
Hague Uholanzi.
0 comments:
Post a Comment