Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
(فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُواْ لِي وَلاَ تَكْفُرُونِ)
(Basi nikumbukeni Nitakukumbukeni, na nishukuruni wala msinikufuru) [Al-Baqarah: 153]
Je,
kuna mbora zaidi ya Mola wetu Mtukufu tunayemhitaji Atukumbuke? Bila
shaka hakuna, kwani Yeye Ndiye tunayemhitaji kwa mambo yetu yote ya
maisha, duniani na Akhera. Hivyo basi tujitahidi kumkumbuka hasa katika
miezi hii mitukufu.
Naye (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametuamrisha tumkumbuke sana
kila wakati kwani Yeye Ndiye Anayeturuzuku neema na fadhila zote. Naye
Anatupa moyo na matumaini kuwa, tutakapomkumbuka Naye Atatukumbuka,
Atazidi kutuongoza, Atatuswalia (Atatupa rehema Zake) Yeye na Malaika Wake, na Atatulipa malipo mema mengi duniani na Akhera. Anasema (Subhaanahu wa Ta'ala):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّهَ ذِكْرًا كَثِيرًا ﴿41﴾ وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا ﴿42﴾
هُوَ الَّذِي يُصَلِّي عَلَيْكُمْ وَمَلَائِكَتُهُ لِيُخْرِجَكُم مِّنَ
الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا ﴿43﴾ تَحِيَّتُهُمْ يَوْمَ يَلْقَوْنَهُ سَلَامٌ وَأَعَدَّ لَهُمْ أَجْرًا كَرِيمًا ﴿44﴾
(Enyi mlioamini! Mdhukuruni Allaah kwa wingi wa kumdhukuru) (Na mtakaseni asubuhi na jioni) (Yeye na Malaika Wake ndio Wanakurehemuni ili kukutoeni gizani mwende kwenye nuru. Naye ni Mwenye kuwarehemu Waumini) (Maamkiano yao siku ya kukutana Naye yatakuwa: Salama! Na Amewaandalia malipo ya ukarimu) [Al-Ahzaab: 42-44]
'Aliy bin Abi Twalhah ameripoti kuwa Ibn 'Abbaas (Radhiya Allahu 'anhu) amesema kuhusu Aayah:
(اذْكُرُوا اللَّهَ ذِكْرًا كَثِيرًا)
((Mdhukuruni Allaah kwa wingi wa kumdhukuru))
"Allaah
Hakuwaamrisha waja Wake kutekeleza wajibu wowote bila ya kuweko mipaka
iliyojulikana na Hupokea nyudhuru za wale wasioweza kutekeleza (wajibu
huo). Ama kumdhukuru Allah, Hakuweka mipaka na hakuna atakayekuwa na
udhuru wa kutokuweza kumdhukuru Allaah isipokuwa atakayedhalilika kwa
kupuuza na kudharau, kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:
(فَاذْكُرُواْ اللّهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَى جُنُوبِكُمْ)
(basi mkumbukeni Allah mkisimama, na mkikaa, na mnapojinyoosha kwa kulala) [An-Nisaa:103]
Kwa
maana; usiku na mchana, katika ardhi kavu au baharini, safarini au
kubakia nyumbani, katika hali ya utajiri au umasikini, katika hali ya
maradhi au katika siha, kwa siri au hadharani – katika hali zote na
mazingira yoyote, Allah Anasema:
(وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا)
(Na mtakaseni asubuhi na jioni)
Mkifanya hivyo Yeye na Malaika Wake Watatuswalia" [At-Twabary 20:280]
Swalah ya Allaah kwa waja Wake ina maana: Anawasifu waja Wake kwa Malaika na pia maana nyingine ni Rahma.
Swalah kutoka kwa Malaika ina maana: ni du'aa zao na kutuombea maghfirah.
Na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(يقول
الله تعالى : أنا عند ظن عبدي بي ، وأنا معه إذا ذكرني ، فإن ذكرني في
نفسه ذكرتهُ في نفسي ، وإن ذكرني في ملأ ذكرته في ملأ خير منهم ،وإن تقرب
إلى شبراً تقربت إليه ذراعاً ،وإن تقرب إلي ذراعاً تقربت إليه باعاً ، وإن
أتاني يمشي أتيتهُ هرولة) البخاري و سلم
(Allaah
Anasema: Mimi niko mbele ya dhana ya mja Wangu Kwangu, akinitaja moyoni
Nami Ninamtaja moyoni na akinitaja katika kundi, Nami Namtaja katika
kundi bora zaidi ya hilo lake, na akijikurubisha Kwangu paa moja, basi
Mimi Najikurubisha kwake kiasi cha dhiraa, na akijikurubisha Kwangu
kiasi cha dhiraa, basi Mimi Nitajikurubisha kwake kiasi cha kunyoosha
mkono hadi kati ya kifua, na akinijia kwa mwendo mdogo basi Nami
Nitamjia kwa mwendo wa kasi) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Maonyo Ya Kughafilika kumdhukuru Allaah
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amewaonya wale ambao nyoyo zao zimeghafilika na kumkumbuka:
(فَوَيْلٌ لِّلْقَاسِيَةِ قُلُوبُهُم مِّن ذِكْرِ اللَّهِ أُوْلَئِكَ فِي ضَلَالٍ مُبِينٍ)
(Basi ole wao wenye nyoyo ngumu zisiomkumbuka Allaah! Hao wamo katika upotofu wa dhaahiri ) [Az-Zumar:22]
Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) naye pia ametuonya katika Hadiyth nyingi, tutataja baadhi yake:
(من قعد مقعداً لك يذكر الله فيه كانت عليه من الله ترة ومن اضطجع مضجعاً لم يذكر الله فيه كانت عليه من الله ترة) ابو داود
(Anayekaa
kikao chochote kile asimtaje Allaah katika kikao hicho basi ana dhambi
kutoka kwa Allaah, na anayelala sehemu yoyote ile kisha asimtaje Allaah
wakati wa kuinuka sehemu hiyo basi ana dhambi kwa Allaah) [Abu Daawuud]
وقال صلى الله عليه وسلم (( ما من قوم يقومون من مجلس لا يذكرون الله فيه إلا قاموا عن مثل جيفة حمار وكان لهم حسرة)) ابو داود و أحمد
Na
amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): (Hapana
watu wowote wale wanaosimama katika kikao walichokaa, kisha wasimtaje
Allaah ila watakuwa wanasimama kama mzoga wa punda, na watakuja juta kwa kutomtaja Allaah) [Abu Daawuud na Ahmad]
Bonyeza
hapa upate Kitabu cha Hiswnul-Muslimi kilichokusanya aina nyingi za
Dhikru-Allaah za kila nyakati, kila hali na popote ulipo:
Baadhi ya Dhikru-Allah zenye thawabu nyingi:
Dhikru-Allaah
hizi unaweza kuzisema huku ukiwa unafanya kazi zako; unapoelekea
kazini, unapopika jikoni au kufanya kazi zako nyingine za nyumba, wakati
wowote mahali popote.
Milioni za thawabu
سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ عَدَدَ خَلْـقِه ، وَرِضـا نَفْسِـه ، وَزِنََـةَ عَـرْشِـه ، وَمِـدادَ كَلِمـاتِـه
Subhaana-Llaahi wa Bihamdihi 'Adada Khalqihi wa Ridhwaa Nafsihi, wa Ziynata 'Arshihi wa Midaada Kalimaatih [Taja mara tatu] [Muslim]
“Ametakasika Allah na Sifa njema zote ni Zake, kwa hisabu ya viumbe Vyake, na Radhi Yake, na uzito wa 'Arshi Yake, na wino wa maneno Yake “
Mfano
mmoja tu wa thawabu hizo ni idadi ya viumbe vya Allah. Je viumbe
vingapi viliokuweko duniani tokea kuumbwa Nabii Aadam (‘alayhis-salaam)
hadi siku ya mwisho? Malaika, Binaadamu, Majini, wanyama wakubwa na
wadogo, wa nchi kavu, baharini, angani, miti na mimea ya kila aina
ulimwenguni kote, mbingu, bahari, milima n.k., ni thawabu ngapi hizo mtu atazichuma kutaja maneno hayo tu ambayo hata hayamchukui zaidi ya dakika moja?
Bonyeza kiungo kifutacho upate pia Adhkaar zenye mamilioni ya thawabu:
Maneno mawili yenye kupendwa sana na Allaah (سبحانه وتعالى)
قال النبي صلّى الله عليه وسلّم : ( كلمتان خفيفتان على اللسان ثقيلتان في الميزان حبيبتان إلى الرحمن : سبحان الله وبحمده ، سبحان الله العظيم ) رواه البخاري ومسلم
Amesema
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) (Maneno mawili ni
mepesi mno juu ya ulimi, mazito mno katika mizani, yanapendeza mno mbele
ya Ar-Rahmaan (Mwenye kurehemu) nayo ni:
سُبْحانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ سُبْحَانَ اللهِ العَظِيمِ
Subhaana-Llahi Wa-Bihamdihi Subhaana-Llahi-l-'Adhwiym)) [Ametakasika Allaah na sifa njema zote ni Zake, Ametakasika Allaah Aliye Mtukufu] [Al-Bukhaariy na Muslim]
Thawabu za aina mbali mbali
Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Atakaye sema:
لا إِلهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْد، وهُوَ عَلى كُلِّ شَيءٍ قَديرٌ
Laa Ilaaha Illa Allaah Wah-dahu Laa Shariyka Lahu, Lahul-Mulku Wa-Lahul-hamdu Wa Huwa 'Alaa Kulli Shay-in qadiyr
"Hapana
mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allaah, hali ya kuwa peke Yake Hana
mshirika, ni Wake Ufalme na ni Zake kila sifa njema, na Yeye juu ya kila
kitu ni Muweza" (mara kumi, ni kama thawabu za mtu aliyeacha huru
nafsi nne katika wana wa Ismaa'iyl) [al-Bukhaariy na Muslim]
0 comments:
Post a Comment