HIKI NI MOJA YA VYUO VIKUBWA VYA KUHIFADHI
QUR AAN NCHI AFRIKA KUSINI.
Waislamu nchini Tanzania wametakiwa kuwekeza katika Uislamu ili maendeleo ya kweli yaweze kupatikana.
Wito huo umetolewa na Sheikh Omar Awadh ambaye ni Mwenyekiti wa Idara ya Madrasa D Y C C C alIpokuwa ana zungumza na Munira blog muda mfupi baada ya kuwasili akitoa nchini Afrika Kusini.
Alisema Waislamu wa Afrika Kusini wamewekeza katika Uislamu na maendeleo yake yanaonekana.
"Ndugu mwandishi wa habari,WALLAAH niliyoyaona kwa wenzetu yameuathiri moyo wangu kwa kiasi kikubwa,wenzetu japo ni wachache lakini wapo mbele katika kuutumikia Uislamu,wamewekeza vya kutosha,wana ardhi kubwa sana,wamejenga vyuo vikubwa vikubwa kwa ajili ya kuhifadhisha Qur aan na na elimu ya dini.
Sheikh Omar ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Muniira Madrasa And Islamic Propagation Association ameendelea kusema,amewakuta watoto wadogo wa kutoka mataifa mbalimbali,ikiwemo tanzania wakipatiwa elimu.
"Nilifarijika kuwakuta watoto wa mataifa mbalimbali hasa watanzania,tena wapo kutoka mikoa mbalimbali,nilikaa na kuongea nao,wamenithibitishia wana pata elimu mzuri na huduma mzuri kwa ujumla".alisema kwa furaha.
Hakusita kutoa wito kwa Waislamu nchini kuhakikisha kila mmoja kwa nafasi yake anawekeza katika uislamu.
"Sisi (waislamu) tupo wengi kuliko Waislamu wa Afrika Kusini kama kila mmoja wetu atawekeza kwa nafasi yake katika dini hakuna kitakachotuzuwia kupata maendeleo",alisema.
Aliongeza kusema kwamba "Tanzania hatuna chuo kikubwa chenye kuhifadhisha na kufundisha Uluumid Diin (elimu ya dini) bali tuna mashule mengi yanayofundisha elimu mchanganyiko,sasa ifike wakati tuwe na vyuo vikubwa vikubwa vinavyo hifadhisha na kufundisha Uluumid Diin ili pia tuwarahisishie watoto wetu kupata elimu pasipo kwenda nje".
Ziara hiyo ya wiki moja ilimuhusisha pia sheikh Hussein Rashid na Sheikh Ally Kubet ilifanyika katika miji ya Darban na Johanesubrg chini ya mwaliko wa WATERVAL ISLAMIC INSITUTE ya Afrika Kusini,kwa na lengo la kujifunza mambo mbalimbali.
PATA HABARI KWA NJIA YA PICHA JUU YA BAADHI YA VYUO VYA KUHIFADHISHA QUR AAN NCHINI AFRIKA KUSINI.
KULIA NI SHEIKH ALLY KUBEIT,OMAR AWADH NA HUSSEIN RASHID
HILI NI ENEO LA KULALA WANAFUNZI
0 comments:
Post a Comment