Oct 19, 2013

MISAADA YAHITAJIKA SYRIA


Moadamiyet, kitongoji cha Damascus


Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na msaada wa dharura, , Valerie Amos, ametoa wito mapigano yasitishwe katika kitongoji cha mji mkuu wa Syria, Damascus, ili kuruhusu chakula na madawa kupelekwa.

Alisema ingawa watu maelfu walikihama kitongoje cha Moadamiyet, juma lilopita, hata hivo maelfu bado wamenasa.

Matamshi yake yanafanana na yale ya wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Marekani, ambayo iliitaka Syria iruhusu msaada wa dharura ufikishwe vitongoji - vitongoji vinavyodhibitiwa na wapiganaji na ambavyo vimezingirwa na jeshi la serikali.

Katika tukio jengine, wanaharakati wanasema kuwa wanajeshi kama 16 wameuwawa kwenye mripuko wa bomu lilotegwa kwenye gari katika kitongoji cha Jaramana, ambacho ni kitiifu kwa Rais Assad.

0 comments:

Post a Comment