Mshambuliaji wa kujitolea mhanga amejiripua kwenye mkahawa uliojaa watu katika mji wa Beledweyne, katikati mwa Somalia.
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Al Shabab, limesema limefanya shambulio hilo.
Serikali ya Somalia, ikisaidiwa na kikosi cha wanajeshi kutoka nchi kadha za Afrika, inapigana na Al Shabab ili kuidhibiti nchi.
Al Shabab imesema iliwalenga wanajeshi kutoka Ethiopia na Djibouti walioko Beledweyne, lakini walioshuhudia tukio hilo wamesema kwamba waliouwawa wengi walikuwa raia.
0 comments:
Post a Comment