Sep 29, 2013

Msikiti Hatarini Kukosa Waumini

HII NDIYO MASJID KAWTHAR

 Ikiwa mijini kuna misikiti yenye kuvutia na inayofurika waumini,hali ni mbaya kwa misikiti iliyo pembezoni mwa miji.

   Hayo yameshuhudiwa leo hii na munira blog baada ya kuutembelea Masjid Kawthar uliopo Kibamba Hosptali.
   
   Akiwa ni mmoja miongoni mwa waumini watano walioidirki swala ya adhuhuri katika msikiti huo,alijionea hali isiyoridhisha katika mazingira ya ndani ya msikiti huo.

   Hata hivyo baada ya swala hiyo mwandishi wetu aligunduwa kwamba katika waumini watano walioswali hapo watatu (akiwemo mwandishi) ni wapita njia tu.

   Ilimlazimu mwandishi wetu kumtafuta Sheikh wa eneo hilo ambapo  (Sheikh Abdul Azizi Ally) alikiri kwamba baadhi ya nyakati wanaswali waumini watatu ijapokuwa kwa Swala ya Ishaa idadi inakuwa kubwa na kufikia kumi na tano.

   "kwa kweli hali hii ni nafuu kabisa,miaka mitatu niliyofika hali ilikuwa mbaya sana,nikaona jambo lakwanza nifanye sensa,al hamdu lillaah tukagundua eneo hili lina waislamu miatano na sitini (560) hii ni watu wazima tu"alisema .

   "Tuna kusudia tuurudie tena mtindo wa kuwapitia waumini majumbani kwao ili tuwalinganie,lakini pia wahadhiri kutoka mjini waje kufanya mihadhara"mwisho wa kumnukuu.

   Aliendelea kusema "Idadi hiyo inatofautiana kabisa na mahudhurio ya waumini msikitini kwetu,kwa kweli ni mtihani,ndugu mwandishi tuna changamoto nyingi sana,kwetu ni kawaida usiku kuswali kwa kutumia mshumaa,kwani inafikia hatua hatuwezi kununua Umeme wa Luku".

   Wakati huo huo sheikh Abdul Azizi Ally alisema wanayo madrasa yenye wanafunzi 136,japo tatizo kubwa lipo katika ulipaji wa ada,

   "Ndugu mwandishi katika mwezi Augost (mwezi wa nane) wanafunzi waliolipa ada ni 21 tu,inasikitisha kuona kwamba watoto wanapenda kusoma,wana moyo wa kusoma na wana akili ya kusoma,lakini wazazi wapo mbali kuwasaidia",mwisho wa kusikitika kwake.

   Kamera ya munira blog ilibahatika kunasa picha kadhaa zinazoonyesha udini wa nyumba hiyo ya ibada.

   Blog hii inatoa wito kwa wapenda kheri kutoa msaada wa hali na mali.

   Masjid Kawthar ipo wastani wa umbali wa mita mia saba kutoka kituo cha basi cha Kibamba Hospitali.

   Kwa wapenda kheri watakao taka kuwanunulia umeme wa luku waingize katika mita namba 87 85 29 11 44 8.



SHEIKH ABDUL AZIZ ALLY AMBAYE  NI IMAMU WA MASJID KAWTHAR

 PINDI WAKISHINDWA KUNUNUA UMEME WANATUMIA MSHUMAA

 SEHEMU KADHAA HAZINA MABUSATI WALA MAZULIA

 PAA HALINA CELLING BOARD


HII NI SEHEMU YA KUTAWADHIA IKIWA IMECHIMBIKA CHIMBIKA

0 comments:

Post a Comment