Oct 2, 2013

Abambwa na Noti Bandia

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia mtu mmoja, Bakari Semkumba (56), mkazi wa Kitopeni wilayani Lushoto, Mkoa wa Tanga kwa kukutwa na noti bandia 304 za sh 10,000,  zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 3.

Akizugumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Urlich Matei amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

Kamanda Matei alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa wakati alipokwenda katika duka moja lililopo Chalinze kwa lengo la kununua maji na kutoa noti bandia ya sh 10,000.

Alisema baada ya mtuhumiwa huyo kutoa noti hiyo ya bandia, muuzaji aliipokea na kuitilia shaka juu ya uhalali wake na kisha kutoa taarifa kwa askari polisi ambao walikuwa karibu na duka hilo.

“Baada ya muuzaji huyo kubaini kwamba noti hiyo ni bandia, alitoa taarifa kwa askari wetu, ambao walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na walipomfanyia upekuzi walimkuta na noti nyingine bandia alizokuwa amezihifadhi  kwenye bahasha tatu tofauti,” alisema Kamanda Matei.

0 comments:

Post a Comment