Sep 29, 2013

Tuwasaidie Vijana Wetu Kufuzu Mitihani.



 PROFESA LIPUMBA AKIHUTUBIA KATIKA MAHAFALI YA WAKHITIMU WA KIISLAMU KIDATO CHA NNE.
HAFLA HIYO ILIFANYIKA JANA KATIKA SHULE YA KAMBANGWA.

Wazazi na walezi nchini wametakiwa kujenga mazingira yatakayo wasaidia watoto wao kufanya vizuri katika mitihani.

Hayo yamesemwa na Bingwa wa Uchumi Duniani Profesa Ibrahim Lipumba alipokuwa anawahutubia wazazi,walimu na viongozi mbalimbali katika mahafali ya wakhitimu wa kidato cha nne kwa wanafunzi wa kiislamu.

Katika hutuba yake iliyodumu kwa dakika ishirini na moja,alitumia muda mfupi kuwahamasisha wakhitimu hao kwa kueleza siri ya mafanikio yake katika sekta ya elimu.

Profesa Lipumba ambaye pia ni Mwnyekiti wa Chama cha Wananchi CUF alisema mbali ya mambo mengine lakini ukaribu na juhudi za wazazi wake katika kumsimamia kielimu ulichangia sana mafanikio yake.

"Wazazi na wadau wa elimu hapa nchini,tuweke utaratibu wa kuwasaidia vijana wetu ili wafanye vizuri katika mitihani yao.mwisho wa kumnukuu.

Miongoni mwa mambo ya kufanya ni pamoja kukifanyia kazi kilio cha vijana wetu cha kuwajengea maktaba ya wanafunzi wa Kiislamu.

"Kwa upande wangu nachangia shilingi laki moja kama chachu ya harakati za ujenzi wa maktaba hiyo,naomba wadau mbali mbali tuwasaidie vijana wetu kwa hali na mali"mwisho wa kumnukuu.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wakhitimu wenzake,Amiri wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu Shuleni hapo (Kamuso) Ustaadh Mwinyi alisema sehemu ya matokeo yasiyo ridhisha katika somo la Maarifa ya Kiislamu,ni kwa kukosekana maktaba ya wanafunzi wa Kiislamu. 

Mahafali ya wakhitimu wa kidato cha nne kwa wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Kambangwa yalifanyika jana ambapo mgeni rasmi Profesa Lipumba,aliwakabidhi vyeti wakhitimu wanaume,huku Bi Aisha Sururu (Diwani wa kuteuliwa kata ya kariakoo) akiwakabidhi vyeti wakhitimu wa kike.
AMIR WA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA KIISLAMU SHULENI KAMBANGWA(KAMUSO) USTAADH MWINYI AKISOMA RISALA.

MMOJA WA WAKHITIMU HAO AKIPOKEA CHETI KUTOKA KWA MGENI RASMI. 
MMOJA WA WAKHITIMU UPANDE WA WASICHANA AKIPOKEA CHETI KUTOKA KWA BI AISHA SURURU.
MGENI RASMI PROF LIPUMBA AKIHAKIKI KWA UMAKINI MKUBWA CHETI KABLA YA KUMKABIDHI MUKHITIMU MUHUSIKA

BAADHI YA WAKHITIMU WA KIUME MUDA MFUPI KABLA YA KUFANYIKA MAHAFALI HAYO JANA.

"AL HAMDU LILLAAH JUKUMU LETU TUMELIMALIZA",NDIVYO ANAVYOONEKANA USTAADH KHALID AKIMWAMBIA MWENZAKE AMBAO WOTE WAWILI WALIKUWA NI WALIMU WA SOMO LA MAARIFA YA UISLAMU SHULENI HAPO" KATIKATI YAO NI AMIR WA WANAFUNZI WA KIISLAMU SHULENI HAPO USTAADH MWINYI.
BAADHI YA WAKHITIMU WASCHANA MUDA MFUPI KABLA KUAFANYIKA MAHAFALI HAYO

0 comments:

Post a Comment