Aug 11, 2013

TUWE NA UMOJA WA KIVITENDO-PROF LIPUMBA.


Na mwandishi wetu wa munira.
Waislamu nchini wametakiwa kuwa na umoja wa kivitendo badala ya umoja wa maneno ambayo hayana mafanikio ya kweli.

Wito huo umetolewa na mchumi bobezi duniani ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF alipokuwa anawahutubia Waislamu waliofurika katika Baraza la Iddi liliofanyika juzi katika Msikiti wa Kichangani Magomeni Mapipa jijini Dar es salaam.


Amesema "ifike wakati sasa tuache kuunadi umoja kwa njia ya maneno matupu,sasa tuunadi na tuunyeshe umoja wetu kwa njia ya vitendo zaidi,mimi ni mwenyekiti wa CUF inapotokea nimeitisha maandamano basi na mimi ni lazima nishiriki maandamano hayo,ili kama kupigwa mabomu au virungu na hata risasi nipigwe na wafuasi wangu"

"Itakuwa haina maana hata kidogo kuunadi umoja wa maneno na inapofika katika vitendo kila mtu hubaki na lwake,bila ya hivyo waislamu hatutosikilizwa na serikali",alisema.