KAMANDA WA POLISI MKOA WA MOROGORO SHILOGILE
- AKIRI POLISI KUTAKA KUMKAMATA,
- ADAI BAADA YA KUANGUKA KATIKA MTARO WAISLAMU WAKAMTOROSHA.
- RISASI ZATUMIKA KUWATAWANYA WAFUASI WAKE.
Na mwandishi wetu wa
munira.
Kamanda wa Jesh la Polisi mkoa wa Morogoro Faustine Shilegile amesema bado wanaendelea kumsaka
katibu mkuu wa kamati ya kutetea haki za Waislamu nchini Tanzania Sheikh
Ponda Issa Ponda licha ya hapo jana kutokufanikiwa katika zoezi hilo.
Ameyasema hayo Asubuhi
hii alipozungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu baada ya
kutakiwa na mwandishi wetu afafanue juu ya tukio hilo.
“Ni kweli tulikuwa tunamfuatilia tangu tuliopata taarifa ya kwamba yupo
katika mhadhara hapa morogoro,lakini tukashindwa kumkamata ndani ya mhadhara
huo,ndipo alipoondoka tukaanza kumfuatilia na hatua chache baadae tukamsimamisha
kwa lengo la kumkamata lakini likatokea kundi kubwa la Waislamu wakazuwia zoezi
hilo na kumtorosha,sasa madai kwamba kapigwa risasi siyafahamu kwa kuwa
hatujamuona bado”mwisho wa kumnukuu.
Alipotakiwa kuelezea
kama jeshi la polisi halikutumia silaha yoyote katika zoezi hilo,kamanda Shilegile alikiri jeshi
la polisi kupiga risasi,”hilo ni kweli
tulipiga risasi baridi kwa lengo la kuwatawanya watu,Sheikh Ponda akaangukia
katika mtaro mara wenzake wakambeba na kumtorosha na kumpeleka hospitali ya
mkoa wa morogoro,lakni cha kushangaza tulipofika hospitali ya mkoa tukaambiwa
mara tu baada ya Sheikh Ponda kufikishwa hapo walimuondoa bila ya kuonwa na
daktari kwa hiyo hatujuwi alipo na tunaendelea kumsaka”
Awali blog hii
iliwasiliana kwa njia ya simu na IGP lakini simu yake ilipokelewa na Coplo Vecent
ambaye alimuelekeza mwandishi wetu awasiliane na msemaji wa Jeshi la Polisi makao makuu ambaye
naye akatoa ushirikiano mzuri wa kumpata kamanda wa polisi wa Mkoa wa Morogoro.