TUFUNGE KWA IKHLAASW-NAIBU KADHI MKUU
- SIYO MWEZI WA MATUMIZI YA FUJO,
- IKHTILAFU YA MUANDAMO WA MWEZI HAIEPUKIKI.
Na mwandishi wetu wa munirablog;
Naibu Kadhi Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)
Sheikh Abuubakar Zubeir amewaasa Waislamu kuutumia vizuri mwezi wa Ramadhani
kwa kufunga kwa Ikhlaswi na si
vinginevyo.
Ameyasema hayo mapema leo hii alipokuwa anazungumza kwa njia
ya simu na mwandishi wa munirablog yenye makazi yake magomeni makuti jijini
dare sa laam.
Alisema nikiwa ni kiongozi wa Dini ya Kiislamu ninadhimma ya
kuwakumbusha Waislamu juu ya umuhimu wa kuutumia vizuri mwezi wa Ramadhani,kikubwa
tuupokee mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kushikamana na uchamungu na tukamilishe
yote ambayo yanayotakikana kufanywa na mfungaji.
“Funga ni Darsa kubwa sana ambalo kwa mwaka tunaletewa mara
moja tu,kupitia Darsa hili la Ramadhani tunajifunza Ucha Mungu,Akhlaaq (tabia
njema) Maadili,Mshikamano,Subra na kuhurumiana,kwa kukaa na njaa (swaumu)
inamfanya hata tajiri ahisi adha ya njaa hivyo inamlainisha moyo wake na kuwahurumia
wale wasio na uwezo,sasa mafundisho haya tunatakiwa tuendelee kuishi nayo hata
baada ya Ramadhan”mwisho wa kumnukuu.
Hakusita kuwaasa Waislamu juu ya kuwa na nidhamu ya matumizi mazuri
ndani ya mwezi huu.”huu sio mwezi wa matumizi ya fujo (israaf) uislamu umekataza matumizi
mabaya pale Mtume S.A.W.aliposema mwenye kutumia kwa wastani Mwenyezi Mungu atamtajirisha
na mwenye kutumia kwa fujo Mwenyezi Mungu atamfukarisha”mwisho wa
kumnukuu.
Kwa upnde mwengine mwandishi wa munirablog alitaka kujuwa
msimamo wa Bakwata kuhusiana na tofauti ya mwezi hasa katika kipindi hiki.
Naibu Kadhi Mkuu alisema,tofauti ya machomozo ya mwezi
haiepukiki,daima hatuwezi kufunga pamoja jambo ambalo hata elimu ya Jiografia
inakiri.
Alizidi kusema “Sisi Bakwata tunasimama na mafundisho ya Mtume
s.a.w aliyesema fungeni kwa kuuona na fungueni kwa kuuona mwezi,lakini Mtume S.A.W akaweka
wazi kwamba pindi huo mwezi ukijicha kwa sababu ya mawingu basi
timizeni siku thelathini (siyo kuutafuta kwa vyombo vya kisanyansi),tena nikupe
faida mwandishi wa habari kwamba hata vitabu vikubwa vya Hadithi kama Swahihil
muslim,Bukhaar,Sunan Abii Dauwd na vinginevyo wanakiri kwamba kila watu (miji)
wanamachimbuko yao,kwa maana watu wafunge kwa kuuona siyo kila mwaka mwezi huo
unaonekana sehemu moja tu”mwisho wa kumnukuu.
“Uislamu ni Dini nyepesi ambayo haimkalifishi mtu afunge hata kama yupo usingizini (muda huo ni usiku) kwa mujibu wa
jiografia yake.”,alisema.
Munirablogspot inawatakia wasomaji wake mfungo mwema wa
Ramadhan.
0 comments:
Post a Comment