WAISLAMU NAWAUSIA MAMBO MATANO-AL ALLAAMA SHEIKH MUHARRAMA
JUMA DOGA.
- PIA ATOA MSIMAMO KUHUSU MUANDAMO.
Na mwandishi wetu wa munirablog.
Waislam nchini
wamepewa nasaha kwa minajili ya kuutumia vyema Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambao
unatarajiwa kuanza masaa machache kama si siku
mbili kutoka leo INSHAA ALLAH.
Nasaha hizo zimetolewa Asubuhi ya leo hii na Al Allaama Sheikh Muharram
Juma Doga alipokuwa anazungumza na mwandishi wa munirablog alipomtembelea
ofisini kwake katika shule ya Al Haramain Jijini Dar es salaam.
Amesema “huu ni mwezi
ambao tunatarajia kila mwenye madhambi yake,ALLAAH atamfutia basi nachukuwa
fursa hii kupitia chombo chako (munirablogspot)ambacho
kimeaanza kutegemewa na Waislamu kuwausia ndugu zangu mambo matano”.mwisho
wa kumnukuu.
Kwanza kila muislamu afahamu ya kwamba umri ni dhamana ya
Mwenyezi Mungu,hivyo ni muhimu kujiibiidisha na ibada sambamba na kuomba
Maghfira ili Ramadhan ikiisha nasi tuwe tumepata msamaha wa ALLAAH,itakuwa ni
khasara Ramadhan inakwisha na bado tumebakiwa na mizigo yetu ya madhambi,alisema.
Aliendelea kusema kwamba jambo la pili ni tusamaeheane,kwani
msamaha ni kitengo kikubwa sana
katika uislam,tujuwe kwamba hakuna mkamilifu ila ALLAAH pekee.
Jambo la tatu tuache migogoro binafsi na tuendelee na Uislamu
wetu uliotukusanya.
Jambo la nne “tumuombe Mungu atuhifadhie na atulindie Amani
yetu tuliyo nayo,ndugu mwandishi sehemu yoyote isiyo na amani hakuna ibada”
alisisitiza.
Alikhitimisha usia wake kwa kuwataka waislamu kuombeana kheri.
Kwa upande mwengine alipokuwa anajibu swali la mwandishi wa munirablog
aliyetaka kujuwa juu ya msimamo wake kuhusu tofauti ya muandamo wa mwezi,Sheikh
Doga alisema,Ulimwengu ni mmoja,hakuna
mwezi zaidi ya mmoja,hivyo basi pale unapoonekana sehemu moja ni jukumu la
waliouona kuwafahamisha wengine wa dunia mzima ili na wao wafunge,msimamo wangu
ndiyo msimamo wa abuu Hanifa,Imam malik,Imam Shaffii na Imama Ahmad,wao kwa
kwa pamoja walishikamana katika msimamo huo japo wafuasi wao walitofautiana,mwisho
wa kumnukuu.
0 comments:
Post a Comment