Jul 10, 2013



MFUNGO WA RAMADHANI WAANZA:
  • WAISLAMU WAFURIKA MISIKITINI.
  • BEI ZA FUTARI ZAPAA

Na mwandishi wetu wa munirablog.
Hatimaye Waislamu nchini Tanzania wameungana na Waislamu wengine duniani kuanza mfungo wa Ramadhan ambao ni nguzo ya nne kati ya nguzo tano za Uislamu,anaripoti mwandishi wetu.

Hali hiyo imekuja baada ya jana kuandama mwezi 29 Shaaban kwa hapa nchini na kutoa fursa kwa mujibu wa sharia kuanza rasmi mfungo wa Ramadhan.

Mwandishi wa habari hizo aliwashuhudia watu kadhaa wakionyeshana mwezi jana mara baada ya kuzama juu.

"Al hamdu Lillah,mwezi nimeuona mimi mwenyewe,nikamuonyesha mama yangu na nikampigia simu ustaadh Ngota,kwa hakika najisikia fakhari kubwa kuona kwamba mwaka huu tunafunga pamoja kwani nasikia Saudia Arabia jana hawakuuona mwezi hivyo kesho Inshaa Allah tutafunga nao pamoja,namuomba Mungu ajaalie Iddil Fitri tuswali pamoja" alisikika Bi Maryamu Salim Said Chondoma mkazi wa Magomeni Makuti Jijini Dar es salaam alipoongea na mwandishi wa munirablog muda mfupi mara baada ya mwezi kuonekana jana..

Wakati huo huo waandishi wa munirablog leo hii wameshuhudia misikiti kadhaa ikiwa imefurika waumini kwa ajili ya ibada ya swala.

Baadhi ya misikiti hiyo ni pamoja na Msikiti wa Kichangani,Msikiti wa Mtoro na Msikiti wa Qiblatain uliopo kariakoo.

"Kwa hakika ingekuwa tunajazana misikitini kila siku Wallaah ingekuwa raha sana" alisikika muumini mmoja aliyewa anasubiri wenzake wamalize kuswali ilwapate nafasi ya kuswali baada ya msikiti huo kujaa ndani na nje katika swala ya Adhuhuri.

Aidha munirablog imebaini kupanda kwa bei za futari katika masoko mbalimbali ya Jijini Dar es salaam.

Bidhaa zilipanda bei ni pamoja na Tambi,Viazi vitamu,MagimbiNndizi mbivu na Njugu mawe,"kwa kweli mwaka huu naona biashara si mzuri,kwa sababu toka asubuhi hadi sasa nimeuza kiroba kimoja cha tambi wakati miaka ya nyuma hadi muda huu wa jioni ingekuwa nimeshauza viroba kumi" alisema Bwana Muhammaed Said mkazi wa temeke Mwembe Yanga ambaye amedai ameanza biaashara hiyo hapo sokoni Kariakoo tokea mwaka 2000.

Aliongeza kusema kwamba pia wanaumizwa na ushuru wa soko kwani mwaka huu wanatakiwa walipe Shilingi elfu tatu kwa kila siku tofauti na mwaka jana kwa siku wakilipa Shilingi elfu moja.

Shamimu Juma mfanya biashara wa sokoni Kariakoo alisema "wanalazimika kuuza viazi mbatata kwa bei kubwa kutokana na wao kuuziwa bei kubwa,"ndugu mwandishi leo nimekwenda kununua viazi gunia moja ni elfu tisini badala ya elfu themanini na tano,sasa hatuna jinsi zaidi ya kuongeza bei japo kidogo" maneno hayo yaliungwa mkono na Bwana Rajabu Chande mkazi wa Mbagala ambaye ni muuzaji wa ndizi mbivu,viazi vitamu na magimbi.

Munira blog imegundua bei za viazi vitamu ni kati ya elfu mbili hadi elfu nne kwa fungu wakati bei ya ndizi mbivu moja ni kati ya 350 hadi 500.

Baadhi ya wafanya biashara wasio muogopa ALLAAH wamekuwa wakitumia kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan kupandisha bei baadhi ya bidhaa na kuwasababishia ukali wa maisha wafungaji.

HAWA NI BAADHI YA WAISLAMU WAKISWALI NJEE YA MSIKITI BAADA YA NDANI KUJAA KAMA WALIVYOKUTWA NA MPIGA PICHA WETU

 
**************************************************************************************************************
 HAWA NI BAADHI YA WAFANYA BIASHARA WAKIWA NA BIASHARA ZAO KAMA WALIVUONASWA NA KAMERA YA MWANDISHI WETU LEO JIONI.


0 comments:

Post a Comment