PASOFA CAMP
WAUKARIBISHA MWEZI
MTUKUFU WA RAMADHAN.
- SHEIKH KWANGAYA AHIMIZA KUMPENDA MTUME S.A.W
- TAASISI YA MUNIIRA MADRASA YAGUSWA NA KUWAZAWADIA VITABU
Na mwandishi wetu wa munirablog
Imezoeleka kwamba makemp (Camps) mbalimbali imekuwa ni
kichaka cha vijana kufanya uhalifu na uchafu mbalimbali ikiwemo mmomonyoko wa
maadili,lakini hali hiyo ni kinyume kabisa kwa PASOFA CAMP ya Magomeni Makuti Jijini
Dare s salaam baada ya jana usiku kufanya hafla fupi ya kuukuaribisha mwezi
mtukufu Ramadhan.
Hafla hiyo iliyofanyika katika mtaa wa Kisangiro iliambatana
na kumswifu Mtume S.a.w
(Mulid) ambapo Madrasa mbalimbali zilihudhuria na kuimba Qaswida
zenye ujumbe maridhawa.
Akiongea na mwandishi wa munirablog,Katibu Mkuu wa
PASOFA CAMP (Pamoja Sote ni Familia) Faqihi Issa alisema “Camp yetu ni tofauti kabisa na
Camps nyengine,sisi tunajishuguhulisha na kukataza mabaya na kuamrisha
mema,lakini pia tunajishughulisha na kusaidiana sisi kwa sisi kwa mambo ya
huzuni au afuraha”mwisho wa kumnukuu.
PASOFA CAMP imeanzishwa mwaka 2003 na sasa inawanachama 33
wanaume watupu,”Sehemu kubwa ya
wanachama wetu walikuwa ni wanafunzi wa Madrasat Mujitahida chini ya Ustaadh
Ahmad Mcheni katika miaka ya tisini kwa hiyo tunawatoa wasiwasi jamii sisi sio
kemp za kihuni hivyo wasisite kutuunga mkono”alisisitiza.
Awali akizungumza katika hafla hiyo,Mhadhiri mwenye mvuto
kwa vijana Sheikh Ramadhan Kwangaya aliwaasa Waislamu kuwa na utamaduni wa
kumpenda Mtume Muhammad S,A,W.
“Ndugu zangu
waislamu,tukae tukifahamu,hakuna chenye thamani katika ulimwengu huu kama
kumpenda Mtume s.a.w.,ukimpenda mtume kwa dhati kabisa,kwanza utamfuata,kaini
pia hautokubali kuona Mtume wako anasemwa vibaya au anadhalilishwa kwa namna
yoyote,nawaomba tuonyeshe mapenzi yetu kivitendo”mwisho wa kumnukuu.
Katika hatua nyengine,Taasisi ya Muniira Madrasa And Islamic
Propagation Association ya magomeni makuti,imewazawadia PASOFA CAMP vitabu vya Jifunze Swala za Faradhi kwa njia nyepesi. Kwa lengo la kuwapapanua
kimaarifa.
Zawadi hizo zilikabidhiwa na Sheikh Ramadhan Kwangaya ambae
pia ni Mshauri Mkuu wa Elimu katika Taasisi hiyo.
“Tumeguswa na hatua ya vijana hawa kuwa na Camp yenye malengo ya
kukatazana mabaya na kuamrishana mema,tukaona tuwaunge mkono japo kwa kuwapa
vitabu vichache”alisema ustaadh ally salum jongo ambaye ni mwenyekiti
wa taasisi ya muniira madrasa wakati akiongea na munirablog.
KATIBU MKUU WA PASOFA CAMP FAQIH ISSA AKIPOKEA ZAWADI YA VITABU KUTOKA KWA SHEIKH KWANGAYA,ZAWADI HIYO ILITOLEWA NA TAASISI YA MUNIIRA MADRASA.
KATIKATI NI IMAMU MKUU WA MASJID TAWWAAB YA MAGOMENI MAKUTI USTAADH ABDUL SHAKUUR FADHIL
SHIKH KWANGAYA AKIWA NA BAADHI YA VIONGOZI WA PASOFA CAMP,KUSHOTO NI MLEZI WA CAMP HIYO USTAADH AHMAD MCHENI NA KULIA NI KATIBU MKUU FAQIH ISSA.
0 comments:
Post a Comment