Jul 6, 2013

Uzinduzi wa Msikiti wa Kisasa Na Rais wa Zanzibar


  • TUZITAYARISHE NAFSI ZETU KUUPOKEA MWEZI WA RAMADHAN.
  • KAPTENI CHILIGATI AKUMBUKWA.


Na mwandishi wetu wa munira.
Waislamu wametakiwa kuzitayarisha nafsi zao na kuwa tayari kuupokea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan unaotarajiwa kuanza wiki ijayo Inshaa Allah.

Hayo yamesemwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Dokta Ally Muhammed Shein katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Dakta Mwinyi Hajj Makame.

Akiizindua nyumba ya ALLAH (Masjid Taqw aa) iliopo Ilala Bungoni Jijini Dar es salaam mapema leo hii,Mheshimiwa Rais amesema tufanye juhudi za makusudi kuhakikisha tunaziandaa nafsi zetu kuupokea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambao kiimani nafsi za waja zinakuwa karibu zaidi na muumba,lakini pia tukiruzukiwa kuingia katika mwezi huo basi tujipinde kwa ibada za usiku na mchana,alisema.

Aidha alimpongeza Bwana Yusuf Khamis Yusuf kwa kujitolea na kuujenga msikiti huo wa kisasa,”kwa kweli nimevutiwa sana na juhudi zenu zilizopelekea leo hii kukamilisha ujenzi huu kwa awamu ya kwanza,lakini pia nimefurahishwa na malengo yenu ya kuufanya msikiti huu uwe wa ghorofa tano,sambamba na azma yenu njema ya kuwa sehemu ya uwanja iliyobakia kujenga shule na kituo cha afya,kwani malengo yenu yanakwenda sambamba na malengo ya Uislamu lakini pia ni imani yangu malengo haya yakifikiwa yataimarisha malezi na afya ya watoto wetu”,mwisho wa kumnukuu.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi,Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum aliwapongeza viongozi na mfadhili wa msikiti huo kwa kushirikiana na hatimaye kumaliza ujenzi wa msikiti kwa awamu ya kwanza,”Bakwata inawapongeza kwa kuweza kufikia hatua hii na Bakwata ilikuwa nanyi bega kwa bega kuhakikisha hamukwami katika kupata misamaha ya kodi serikalini na itaendelea kushirikiana nanyi japo katika risala yenu sikusikia mukiishukuru Bakwata”mwisho wa kumnukuu.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Baraza la Wadhamini la Masjid Taq waa Sheikh Rashid Mtambule akisoma risala alimshukuru aliyekuwa waziri wa ardhi mheshimiwa Kapteni John Chiligati.

“Kwa kweli Baraza la Wadhamini linamshukuru Kapteni John Chiligati kwani baada ya kumfikishiia malalamiko yetu dhidi ya hujuma zilikusudia kuwadhulumu waislamu kiwanja hiki hatimaye alikuja  hapa na kuona hali halisi,ambapo bila kujali itikadi yake baada ya siku chache akatupatia hati ya kiwanja,tunamuomba mwenyezi mungu amuongowe na mwishowe auone ukweli wa uislamu”alisema.

Hakusita kuahidi kwamba msikiti huo utadumisha amani na upendo kwa jamii yote inayozunguka eneo hilo bila kujali itikadi yoyote.
Ujenzi wa msikiti huo kwa awamu ya kwanza umegharimu shilingi bilioni moja na milioni mia tatu tisini na tano.

Hafla hiyo imehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini kadhi mkuu na mufti wa Zanzibar,masheikh sambamba na Waziri Maendeleo ya watoto Bi Sofia Simba.

MATUKIO YA UZINDUZI WA MASJID TAQ WAA KATIKA PICHA;


 SEHEMU YA WAUMINI WALIOFURIKA KUSHUDIA UZINDUZI WA MSIKITI MPYA LEO HII MAENEO YA ILALA BUNGONI.


SHEIKH WA MKOA WA DAR ES SALAAM AL HAD MUSSA SALUM AKIMKARIBISHA MGENI RASMI ILI ATOE NASAHA ZAKE.
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR DOCTOR MWINYI HAJI MAKAME AKISOMA HOTUBA KWA NIABA YA RAIS WA ZANZIBAR MHE ALLY MUHAMMED SHEIN.

MWAKILISHI WA MFADHILI ALIYEUJENGA MASJID TAQ WAA AKIPOKEA ZAWADI MAALUM KUTOKA KWA MGENI RASMI AMBAYO IMETOLEWA NA BARAZA LA WADHAMINI WA MSIKITI HUO.

MHANDISI ALIYECHORA RAMANI YA MSIKITI (BILA YA MALIPO) AKIPOKEA ZAWADI ILIYOANDALIWA NA BARAZA LA WADHAMINI WA MASJID TAQ WAA LEO HII.

VIONGOZI WAKIWA WAMESIMAMA KUITIKIA DUA ILIYOSOMWA NA KADHI MKUU WA ZANZIBAR SHEIKH KHAMIS HAJJ KHAMIS IKIWA NI ISHARA YA KUMALIZA HAFLA YA UZINDUZI WA MSIKITI HUO LEO HII.

 KWA NIABA YA RAIS WA ZANZIBAR,MHE WAZIRI AKIFUNGUA PAZIA KUASHIRIA KUZINDUA MSIKITI HUO.


 ANAONEKANA MHE WAZIRI AKISEMA BISMILLAAH RAHMAN RAHIIM WAKATI ANAFUNGUA MLANGO WA MSIKITI WA TAQ WA LEO HII.
HAPA MHE WAZIRI KWA NIABA YA RAIS WA ZANZIBAR ANAKUWA NI MTU WA KWANZA KUINGIA MSIKITINI MARA NAADA YA KUUZINDUA NA KUUFUNGUA MASJID TAQ WAA ULIOPO ILALA BUNGONI JIJINI DAR ES SALAAM,LEO HII BAADA YA HAPO MHE WAZIRI ALISWALI SWALA YA ADHUHRI PAMOJA NA MAMIA WISLAMU WALIOHUDHURIA HAFLA HIYO.

HUU NDIYO MASJID TAQ WAA AMBAO NI MSIKITI WA KISASA ULIOZINDULIWA LEO HII NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS MHE MWINYI HAJ MAKAME KWA NIABA YA RAIS WA ZANZIBAR.

0 comments:

Post a Comment