Jul 4, 2013

Home



RAIS WA ZANZIBAR KUUZINDUA MSIKITI ILALA.

  •  UMEJENGWA NA MZALENDO.
Na mwandishi wetu wa munirablog.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Dokta Ally  Muhammad Shein,anatarajiwa kuuzindua Masjid TAQ-WAA uliopo lIala Bungoni Jijini Dar es salaam.



Akiongea na munirablog kwa njia ya simu leo mchana,Sheikh Abdul Wakati Abdul ambae pia ni Imamu Mkuu wa msikiti huo amesema uzinduzi huo utafanyika Jumamosi ya tarehe 7 mwezi wa saba kuanzia saa nne asubuhi Inshaa allah.



Aliendelea kuipasha blog ya munira kwamba kutakuwa na matukio mbalimbali yatakayoambatana na uzinduzi huo ikiwemo utenzi,mawaidha kutoka kwa masheikh mbalimbali akiwemo Sheikh Abdul Qaadir wa Temeke ambapo hafla hiyo itakhitimshwa mara baada ya Swala ya Adhuhuri,”kwa mujibu wa ratibu mhe Rais atawasili saa tano na dakika ishirini na tutaswali naye Swala ya Adhuhuri Inshaa allaah kisha tutapata dhifa ya pamoja ambapo ndiyo itakuwa mwisho wa hafla yetu”,alisema sheikh wakati



Akijibu swali la mwandishi wa munirablog juu ya sababu zilizowapelekea kumchagua Mhe Shein kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo,alisema “tulifanya shuuraa na majina mbalimbali yalipigiwa kura,lakini jina la Mhe Shein liliibuka mara kadhaa,na hivyo tukakubaliana kwa kauli moja kwamba yeye ndiye apewe dhamana ya kuuzindua msikiti huu ambao umejengwa na mzalendo Bwana yusuf khamis”



Natowa wito kwa waislamu tujitokeze kwa wingi ili tuje kushuhudia nyumba ya ALLAH inavyozinduliwa,kwa hakika hii ni fakhari kwetu na ni uzinduzi wa aina hii ndiyo tunaotakiwa sisi waislamu kukuhudhuria kwa wingi.mwisho wa kumnukuu.



Mwandishi wa munirablog alifanikiwa kufika eneo hilo muda mfupi kabla ya swala ya maghrib leo hii na kuushuhudia msikiti huo namna ulivyokuwa mzuri (Maa shaa ALLAH) huku akiwakuta mafundi wakiwa katika hatua za mwisho za kufanya usafi.



 HUU NI MASJID TAQ-WAA ULIOPO ILALA BUNGONI AMBAO UNATARAJIWA KUZINDULIWA NA RAIS WA ZANZIBAR MHE DOCTOR ALLY MUHAMMAD SHEIN JUMAMOSI YA TAREHE 7 JULY INSHAA ALLAH.



0 comments:

Post a Comment