Wabunge wa kaunti ya Isiolo, wamelishana makonde mbele ya umma,
baada ya kutofautiana vikali kuhusu tarehe rasmi ya ufunguzi wa vikao
vya bunge la kaunti hiyo mwaka huu.
Duru za kuaminika zinaarifu kuwa kumekuwa
na tofauti kali kati ya gavana godana Doyo, na spika wa bunge hilo
Mohamed Tubi kuhusu tarehe ya ufunguzi rasmi ya Bunge hilo mwaka huu.
Tubi ambaye ni spika wa bunge hilo amesema
kuwa bunge hilo linafaa kufunguliwa wiki ya pili ya mwezi februari huku
gavana akitaka bunge hilolifunguliwe hii leo jambo ambalo baadhi ya
wabunge wamepinga vikali.
Makundi hayo mawili yamekuwa yakitofautiana
vikali kuhusu uongozi wa kaunti hiyo,huku wabunge wanaounga mkono spika
wakidai kuwa gavana anania ya kukandamiza majukumu ya wabunge hao.
Feb 4, 2015
Wabunge watwangana makonde
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment