Feb 4, 2015

Watanzania wengi hawajui sheria ya Mirathi

 

Malalamiko na maswali kuhusu mirathi na talaka jana yalitawala katika Maonyesho ya Wiki ya Sheria, yaliyohitimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. 

Akizungumza katika maonyesho hayo, Jaji Kiongozi, Shaaban Lila alisema Watanzania wengi hawana uelewa wa masuala ya kisheria.
Jaji Lila alisema lengo la maonyesho hayo lilikuwa ni kuwafafanulia wananchi kuhusu huduma na taratibu za utendaji wa Mahakama.
Msimamizi wa Kitengo cha Masuala ya Mirathi katika maonyesho hayo, Janeth Mwanisau alisema wanawake wengi walijitokeza hususan wajane. Alisema kutokana na unyeti wa tatizo la mirathi, ndiyo maana limetenganishwa na masuala mengine.
“Wanawake wamefika na kuuliza maswali huku wakieleza malalamiko yao ya kutengwa au kutokushirikishwa katika kufungua mirathi,” alisema Mwanisau.
Jaji Mkuu, Mohamed Chande alisema kaulimbiu ya maadhimisho hayo ilikuwa ni ‘Fursa ya kupata haki ni wajibu wa Serikali, Mahakama na wadau wote,’ na ililenga kuongeza uelewa wa wananchi. “Tulichagua kaulimbiu hii kwa sababu tunataka huduma zetu ziwafikie kwa haraka.

 Nimeambiwa wananchi wameuliza maswali mengi ambayo wanasheria tunayaona ya kawaida lakini kwao ni magumu ,” alisema Jaji Chande.

0 comments:

Post a Comment