Feb 16, 2015

VIKUNDI VYA KIMAENDELEO VYA MIKOA VISIGEUKE VYA KIKABILA;MHE MAKAMBA

Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolia Mheshimiwa January Makamba amesema,vikundi vya Maendeleo vya mikoa,visigeuke kuwa ni vikundi vya kikabila.

Tahadhari hiyo ameitoa jana alipokua anawahutubia mamia ya wanachama wa Umoja wa Wakaazi wa Mkoa wa Tanga waishio Dar esalaam (UMATADA).

Mheshimiwa Makamba ambaye pia ni mbunge wa Bumburi Mkoa wa Tanga amesema,kuishi Dar es alaam hakuondoshi uhalali wa kuwa na vikundi vya kuendeleza mikoa yetu tuliyotoka,lakini ni vikundi hivyo visigeuke na kua ni vikundi vya kikabila.

"Nawapongeza sana kwa kuanzisha umoja huu,wenye nia ya kuendeleza mkoa wa Tanga,binafsi nimevutiwa sana na malengo yenu samba mba na juhudi zenu,kuanzia sasa nami najiunga rasmi na umoja huu,na nitawashawishi Wabunge wote na viongozi wa Tanga,ili nao wajiunge na umoja huu",alisema

Aidha aliwataka viongozi na wanachama wa umoja huo kuzikuza pesa zilizopo benk ili kutanua mfuko wa umoja.

"Zamani ilikua ni fakhari kusema kwamba benki tuna milioni ishirini na tano,lakini sasa hali si hiyo,bali jambo la msingi ni kuhakikisha pesa hiyo tunaiingiza katika mzunguko wa kifedha,ambapo ninaamini baada ya miezi michache mutakua na zaidi ya milioni mia moja",mwisho wa kumnukuu.

Awali akisoma risala ya umoja huo,Al haj Abdallah Sabaya alisema,kwa sasa umoja wao una miliki ardhi heka mia moja zilizopatikana kwa juhudi ya mhe Najim (MJUMBE WA NEC CCM TAIFA),pia wanamiliki SACCOS na wana pesa Taslimu Milioni Ishirini na Tano.

Mkutano huo wa mwaka ulifanyika katika viwanja vya Shule ya Al Haramain iliyopo jijini Dar es salaam.




Baadhi ya wana UMATADA wakifuatilia yanayojiri katika mkutano huo.
Mhe Mkamba hakuawaacha nyuma akina mama.
Mheshimiwa Makamba,akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wakuu.

0 comments:

Post a Comment