Jan 18, 2015

MADRASA ZATAKIWA KUANZISHA MIRADI:WITO.

Ustaadh Juma Rashid ambaye ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Waislamu wa Magomeni Makuti,akiongea katika hafla ya Maulid ya kwanza ya pamoja kwa Waislamu wa Makuti,Magomeni Makuti.

Madrasa nchini Tanzania zimetakiwa kuanzisha miradi ili kujikomboa kutoka katika Fikra tegemezi.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Ustaadh Juma Rashid alipokua anatoa Tamko la Jumuiya hiyo.

Amesema kwa miaka mingi Madrasa zimekua wanyonge kiuchumi na kutegemea misaada kutoka kwa watu mbali,zama hizo zimekwisha na sasa tuanzishe miradi ili tunasuke na hali hiyo.

Aidha alikiri kwamba Madrasa zinakabiliwa na hali ngumu ya kimaisha aliyodai kwamba inasababishwa na hali tatu.

Akizitaja sababu hizo,Ustaadh Juma alisema kwamba kwanza ni Madrasa zenyewe kukosa kujitambua na utayari wa kubadilika.

Wazazi na baadhi ya Waislamu kukosa kuziunga mkono licha ya kua na uwezo wa kufanya hivyo,alisema kua hii ni sababu ya pili.

Huku sababu ya tatu akiitaja kua ni mfumo wa mamlaka ya nchi kutokuzitambua Madrasa kama vyombo muhimu,alisema.

Ndugu zangu Madrasa zetu ni viwanda muhimu katika kuzalisha Maadili mema Kwa taifa,lakini pia madrasa zetu zina uwezo wa kutoa ajira na kuchangia pato la taifa,alisema.

"Haya yote yanawezekana iwapo tutajitambua,tutajipanga na kuanzisha miradi inayotokana na rasmi mali watu".mwisho wa kumnukuu.

Aidha alizitaka Madrasa za Magomeni Makuti ziutumie mwaka huu kuzisajili Madrasa zao ili kua na uhuru na wigo mpana wa utendaji.

"Ndugu zangu kwa niaba ya Jumuiya naziagiza Madrasa zote kuelekea Mwaka 2020 uwe ni mwaka wa maadiliko ya kiuchumi katika Madrasa zetu,na kwa kuanzia na hilo mwaka huu 2015 tuhakikishe Madrasa zetu tunazisajili".Alisema.

Aidha alizitaka Madrasa kua na Utamaduni wa kuwashirikisha Wataalamu wa fani mbali mbali katika kufikia malengo yao.

Magomeni Makuti ina Jumla ya Madrasa kumi na Misikiti miwili.

0 comments:

Post a Comment