Jan 17, 2015

Viongozi wa Kisiasa Tuitikie Miito Ya Kidini.Sheikh Kwwngaya

Viongozi wa kisiasa wametakiwa kuitikia miito ya kidini ikiwa ni sehemu ya kuwatumikia wananchi.

Hayo yamesemwa na sheikh na Ramadhani Kwangaya alipokua anawahutubia mamia ya Waislamu waliohudhuria hafla ya maulid ya nayoendelea usiku huu katika viwanja vya barafu Jijini Dar es salaam.

Amesema viongozi wa kisiasa wamekuwa wanakwepa kuhudhuria hafla za kidini hasa za kiislamu,kitu ambacho si sahihi.

Tuhudhurieni,kwani tutajifunza mengi,alisema sheikh kwangaya..

Huku akitoa mifano na visa kadhaa vya mtume Muhammad Saw shekh kwangaya alisema ukiwa kiongozi unapaswa kuonja ladha mbali mbali ya unao waongoza.

Ndugu zako,ukialikwa na hata mafakiri,basi teremka kutoka katika ghorofa,kisha kaa nao katika jamvi,bila shaka yapo utakayo jifunza.alisema.

Kumekua na malalamiko mengi kutoka kwa baadhi ya Waislamu wakidai mialiko mingi ya Shughuli za kiislamu wanayowapelekea viongozi wa ngazi za kiserikali,wengi wao hawahudhurii,tofauti na upande wa pili.

Hafla hiyo ya kwanza kihistoria katika eneo hilo,iliandaliwa na Jumuiya hilo,ya Maendeleo ya Waislamu wa Magomeni.

0 comments:

Post a Comment