Jan 16, 2015

Watanzania Tuienzi Amani.Mhe Idd Azan

Watanzania wametakiwa kuienzi amani kwa kua ndiyo tunu pekee yenye kutoa nafasi ya kufanya kila kitu.

Hayo yamesemwa na Mhe Idd Azan ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,wakati akitoa salamu Kwa waislamu waliofurika katika uwanjawa barafu Jijini Dar es salaam.

Amesema umuhimu wa amani ni kubwa sana bila ya amani hata haya maulid tusingefanya.

Ndugu zangu hivi majuzi tu kulikua na uvumi wa panya road na watu wakaacha Shughuli zao na kuanza kukimbia hovyo,sasa hawa ni panya Road tu,.....hii ni sehemu ya umuhimu wa amani kwetu.mwisho wa kumnukuu.

Aidha aliwataka wananchi waliombee taifa ili katika uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Mwishoni mwa mwaka huu ufanyike kwa amani.

Picha chini ni baadhi ya waumini waliohudhuria hafla hiyo.


0 comments:

Post a Comment